May 25, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mamilioni ya Man United yamuibua MO

Spread the love

 

MKATABA mpya wa udhamini wa jezi waliongia klabu ya Manchester United wenye thamani ya Shilingi 703 bilioni, umemuibua Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya klabu ya Simba, Mohammed Dewji ‘MO’ na kufunguka kuwa Simba haipati hata asilimia moja ya kiasi hiko cha pesa kutoka kwa mdhamini wa sasa. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Simba kwa sasa inadhaminiwa na kampuni ya kubashiri ya SportsPesa ambao walisaini mkataba huo Mei 2017 kwa kipindi cha miaka mitano ukiwa na thamani ya shilingi 4.96 bilioni.

MO amefunguka hayo kupitia ukura wake wa kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter huku akionesha masikitiko yake juu ya mkataba ambao klabu ya Simba waliingia na SportsPesa, akilinganisha na ule waliosaini klabu ya Manchester United ambao wameingia na kampuni ya TeamView ambao wanakuja kuwa mbadala wa Chevrolet ambao ni wadhamini wa sasa.

Mwenyekiti huyo aliandika kuwa Manchester United wamekubali dili lenye thamani ya dola za kimarekani 305 milioni, (sawa na Sh. 703 bilioni), kwa mkataba wa miaka mitano, ambapo Simba haipati hata asilimia moja ya pesa hiyo kutoka kwa mdhamini wa sasa.

Wakati klabu ya Simba inaingia mkataba na kampuni hiyo mchakato wa mabadiliko ya uwendeshaji ndani ya klabu hiyo ulikuwa bado haujakamilika kama ilivyo sasa.

Mkataba kati ya Simba na SportsPesa umebakiza mwaka moja ili uweze kukamilika na huenda kukawa na majadiliano mapya au kuachana nao.

Licha ya kuwa mwekezaji ndani ya klabu hiyo, MO Dewji kupitia kampuni yake ya MeTL ni sehemu ya wadhamini wa klabu ya Simba kupitia bidhaa mbalimbali.

error: Content is protected !!