May 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mama Janeth Magufuli amtoa machozi Rais Samia

Spread the love

 

SIMANZI iliyotanda usoni mwa Janeth, Mjane wa Aliyekuwa Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli (61), amemfanya Rais Samia Suluhu Hassan, kutokwa chozi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Pia, Rais Samia amekuwa akimfariji Mama Janeth ambaye anaonekana mwenye majonzi na kushindwa kukaa vizuri kwenye kiti chake.

Mama Janeth, ameshindwa kujizuia, pindi alipoona msafara uliobeba mwili wa mme wake, Magufuli ukiingia katika Uwanja wa Jamhuri, Dodoma leo Jumatatu, tarehe 22 Machi 2021.

Msafara huo, umeingia uwanjani hapo saa 4:43 asubuhi, ukitoka viwanja vya Bunge, Dodoma ambapo wabunge walipata fursa ya kuuaga mwili wa Dk. Magufuli, aliyefariki 17 Machi 2021, Hospitali ya Mzena, Dar es Salaam.

Msafara mzima, ulizunguka uwanja mzima mara moja huku umati wote wa waombolezaji wakisimama akiwemo Mama Janeth, aliyekaa kushoto mwa Rais Samia.

Mara baada ya msafara huo kusimama eneo ambalo jeneza lenye mwili wa Dk. Magufuli kushushwa, Mama Janeth alionekana kushindwa kujizuia na kulazima kukaa huku Rais Samia, akionekana kushika kitambaa chake na kujifuta.

Baada ya mwili wa Dk. Magufuli kushushwa na kupelekwa eneop maalum ulipoandaliwa na watu wote kukaa huku Mama Janeth akionekana mwenye majonzi akisaidiwa na wasaidizi wake, Rais Samia, alimfariki kwa kumshika mkono wa kulia.

Hata baada ya kushushwa na kupigwa nyimbo wa Taifa na wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, watu wote walisimama huku Mama Janeth, pekee alikuwa amekaa kwenye kiti chake.

Mara kadhaa, Rais Samia amekuwa akimwona Mama Janeth, amekuwa akitoa kitambaa kujifuta machoni mwake.

error: Content is protected !!