December 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mamia wamuaga kaka yake Mbowe

Spread the love

MAMIA ya watu leo tarehe 2 Agosti 2019, wamejitokeza katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Nshara Machame kuuagwa mwili wa Meja Jenerali mstaafu, Alfred Mbowe. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Alfred ni kaka wa Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), mazishi yake yanatarajiwa kufanyika katika Kijiji cha Nshara, Hai mkoani humo.

Meja huyo alifariki dunia tarehe 28 Julai 2019 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) ambapo aliagwa jijini Dar es Salaam tarehe 31 Julai 2019.

Viongozi mbalimbali wa dini, wameshiriki ibada hiyo ambapo jijini Dar es Salaam, Rais John Magufuli, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete na viongozi wengine walipata fursa ya kuuaga mwili wa Alfred (66). Alistaafu jeshi mwaka 2009.

error: Content is protected !!