Wednesday , 29 March 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Mambo matano kuteka mkutano wa faragha wa mawaziri Arusha
Habari za Siasa

Mambo matano kuteka mkutano wa faragha wa mawaziri Arusha

Spread the love

 

KATIBU Mkuu Kiongozi, Dk. Moses Kusikulika, amesema mada tano zitajadiliwa katika mkutano wa faragha wa siku tatu wa mawaziri na makatibu wa wizara, unaofanyika jijini Arusha. Anaripoti Mwandishi Wetu, Arusha … (endele).

Dk. Kusiluka ametaja mada hizo leo Alhamisi tarehe 2 Machi 2023, katika ufunguzi wa mkutano huo uliofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan, jijini Arusha.

Ametaja mada hizo kuwa ni, maelekezo ya Rais Samia kwa watendaji hao wa Serikali, taratibu za uendeshaji, mahusiano na mipaka ya utendaji kazi serikalini, utaratibu wa utoaji maamuzi makubwa ya kisera serikalini na usimamizi wa rasilimali watu na uhusiano wa Serikali na sekta binafsi.

Mbali na mada hizo kuu, Dk. Kusiluka amesema kutakuwa na mada ndogo 17, ambazo zitatolewa na watoa mada 17, akiwemo Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda; Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu, Balozi Ombeni Sefue na Mshauri wa Rais katika masuala ya majadiliano, Prof. Palamagamba Kabudi.

Wengine ni Leonard Msusa, kutoka sekta binafsi. Mtaalamu wa masuala ya rasilimali watu, Zuhura Muro na aliyekuwa Katibu Mkuu Utumishi, Dk, Laurian Ndumbaru.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

TEMESA iliyokarabati Kivuko kwa Bil 7.5 yapata hati chafu

Spread the love  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),...

Habari za Siasa

ACT-Wazalendo yakusanya Mil 8.5/- kodi ya zuio na kutokomea nazo

Spread the love  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),...

Habari za Siasa

DC Kasilda Mgeni ahamasisha chakula shuleni

Spread the love  MKUU wa Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro, Kasilda Mgeni...

Habari za Siasa

Bilioni 223.9 zapelekwa Tunduru ndani ya miaka 2 ya SSH

Spread the love  ZAIDI ya Sh. bilioni 223.9 zimepelekwa Wilaya ya Tunduru...

error: Content is protected !!