Wednesday , 29 March 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Samia awataka mawaziri kujibu upotoshaji
Habari za Siasa

Rais Samia awataka mawaziri kujibu upotoshaji

Rais Samia Suluhu Hassan
Spread the love

 

RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amewataka mawaziri kueleza mafanikio ya Serikali mara kwa mara, ili kudhibiti baadhi ya watu wanaofanya upotoshaji. Anaripoti Mwandishi Wetu, Arusha … (endelea).

Akifungua mkutano wa faragha wa mawaziri na makatibu wakuu wa wizara, leo tarehe 2 Machi 2023, jijini Arusha, Rais Samia amesema viongozi wa umma wamekuwa wazito kusema mafanikio hayo na kuacha watu wengine kuendelea kufanya upotoshaji.

“Nataka kuwakumbusha umuhimu wa kuisemea serikali kama moja ya mawasiliano nje ya Serikali. Katika eneo hili hatujafanya vizuri sana, tumekuwa wazito kuyasemea mafanikio mengi tunayopata na hivyo kuacha watu wengine kuendelea kufanya upotoshaji. Kuna usemi unaosema uongo ukisemwa mara nyingi huwa ukweli,” amesema Rais Samia.

Mkuu huyo wa nchi amesema, kuna mwanasiasa mmoja jijini Arusha, aliwahi kudai kwamba serikali imetelekeza visima vya maji na kutumia fedha nyingi kupeleka maji kwa wananchi, huku akijua kwamba visima hivyo vilikuwa na maji ambayo hayakuwa salama kwa matumizi ya wananchi kwa kuwa yalikuwa na chumvi nyingi hivyo serikali ikaamua kuwapeleka maji baridi wananchi.

“Wizara inayohusika ilitakiwa kusimama haraka na kutoa ufafanuzi na kumueleza kwa nini visima viliachwa,” amesema Rais Samia.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

TEMESA iliyokarabati Kivuko kwa Bil 7.5 yapata hati chafu

Spread the love  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),...

Habari za Siasa

ACT-Wazalendo yakusanya Mil 8.5/- kodi ya zuio na kutokomea nazo

Spread the love  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),...

Habari za Siasa

DC Kasilda Mgeni ahamasisha chakula shuleni

Spread the love  MKUU wa Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro, Kasilda Mgeni...

Habari za Siasa

Bilioni 223.9 zapelekwa Tunduru ndani ya miaka 2 ya SSH

Spread the love  ZAIDI ya Sh. bilioni 223.9 zimepelekwa Wilaya ya Tunduru...

error: Content is protected !!