MAMBO sita yanatarajiwa kutikisa katika vikao vya Kamati za Kudumu za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania vitakavyoanza Januari 19 hadi 29 mwaka huu, ikiwemo kupokea na kujadili taarifa mbalimbali za utekelezaji wa maazimio ya Bunge. Anaripoti Jonas Mushi…(endelea)
Kamti hizo zinakutana kabla ya Mkutano wa 10 wa Bunge uliopangwa kuanza tarehe 31, Januari, 2023.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Alhamisi tarehe 5 Januari, 2023 na Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Kimataifa Ofisi ya Bunge, shughuli zilizopangwa kufanywa na Kamati katika vikao hivyo ni pamoja na kupokea na kujadili Taarifa za Utekelezaji wa Maazimio ya Bunge yaliyotokana na Taarifa za Mwaka za Shughuli za Kamati zilizowasilishwa bungeni Februari, 2022.
Taarifa hiyo pia imeeleza kuwa kamati zitapokea na kujadili taarifa mbalimbali kuhusu shughuli za Umma nchini ili kufuatilia utekelezaji wa sera na mipango ya sekta zinazohusika.
Pia kamati mbili zinazohusika na kusimamia matumizi ya fedha za umma yaani Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) na Kamti ya Hesabu za Seriklai za Mitaa (LAAC), zitakuwa na kibarua cha kuchambua taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kuhusu kaguzi Maalumu na Kaguzi za Ufanisi.
Kazi nyingine itakayofanywa katika kipindi hicho ni kupokea na kchambua taarifa ya uwekezaji wa mitaji ya umma ili kubaini iwapo uwekezaji huo una ufanisi na kuwa umezingatia taratibu, sheria na miongozo mujarabu ya biashara.
Pia kamati zitapokea na kujadili Taarifa kutoka kwenye Wizara na Taasisi mbalimbali kuhusu ukusanyaji wa mapato, usimamizi wa vyanzo vya mapato na utekelezaji wa bajeti.
Aidha Kamati ya Sheria Ndogo itachambua sheria ndogo zilizowasilishwa wakati wa Mkutano wa Tisa wa Bunge sambamba na kupokea na kuchambua taarifa ya utekelezaji wa Maazimio ya Bunge kuhusu Sheria Ndogo ziilizowasilishwa katika Mkutano wa Tano, Sita na Saba wa Bunge.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo kamati mbili zinatarajiwa kuanza shughuli zake mapema zaidi tarehe 9 Januari ikiwemo Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo na Makamati ya Kudumu ya Bunge ya Masuala ya UKIMWI.
Leave a comment