Monday , 11 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Makonda awagawa Watanzania, Karume aishangaa CCM
Habari za SiasaTangulizi

Makonda awagawa Watanzania, Karume aishangaa CCM

Spread the love

UTEUZI wa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, katika nafasi ya ukatibu wa itikadi na uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), umeibua hisia tofauti baada ya baadhi kuupongeza na wengine kuupinga kwa madai kuwa mwanasiasa huyo hana historia nzuri katika uongozi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Mjadala juu ya uteuzi huo uliofanywa na Halmashauri Kuu ya CCM (NEC), uliibuka baada ya kutangazwa jana Jumapili na mtangulizi wa Makonda, Sophia Mjema.

Baada ya mjadala huo kushika kasi, leo tarehe 24 Oktoba 2023, Mtendaji Mkuu wa Kituo cha Sera za Kimataifa Afrika, Omari Mjenga, amesema uteuzi wa Makonda hauna makosa na kwamba umefanyika baada ya CCM kujadili kwa kina kabla ya kufikia uamuzi huo.

“Mimi ninavyokifahamu CCM ni chama kikubwa sana na mpaka uteuzi wa Makonda unafanyika kulikuwa na mashauriano mengi sana, wakakubaliana kwanza. Halijafanyika kosa lakini pia tunaingia katika kipindi cha mavuno mwakani tuna uchaguzi wa serikali za mitaa na 2025 tuna uchaguzi mkuu. Chama cha siasa duniani dhima yake ni kushika madaraka hivyo lazima kiwe na nia na focus kubwa,” amesema Mjenga.

Mjenga amesema kuwa, huenda uteuzi wa Makonda ni sehemu ya utekelezaji wa maonoya Rais Samia ya kufanya mageuzi na upatanishi ndani ya Serikali, na kwamba kwa sasa kuelekea maandalizi ya uchaguzi  mkuu na wa serikali ya mitaa, ameamua kuimarisha maridhiano ndani ya CCM.

“Rais Samia ameona wakati tunaelekea kwenye uchaguzi namhitaji fulani, ni jambo sahihi kabisa halafu Paul ni kijana mdogo bado ana nguvu sana na ushawishi na waliomtangulia wamefanya kazi nzuri umemuona Nape amempongeza,” amesema Mjenga.

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu, kupitia ukurasa wake wa mtandao wa X zamani ukifahamika kama Twitter, aliandika “hongera sana mwenezi wetu taifa, kazi iendelee.”

Naye aliyekuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, ameupongeza uteuzi huo huku akiwajibu wanaoukosoa kwamba, Mungu ameagiza wanadamu wasamehe wanaokosea.

“Mdogo wangu Paul, Karibu sana kwenye Uongozi wa juu kabisa wa Chama chetu. Nina hakika umetumia vizuri muda wa likizo, and now you are ready for the job! hongera kwa kuaminiwa na nakutakia kila la kheri,” ameandika.

Wakati uteuzi huo ukiungwa mkono, baadhi ya watu mashughuli wakiwemo wanasiasa na wanaharakati wameupinga, wakidai kuwa Makonda ana historia mbaya katika uongozi.

Huku wakikumbushia hatua ya Serikali ya Marekani, iliyochukuliwa 2020 ya kumwekea kizuizi cha kuingia nchini humo wakimtuhumu kuhusika na matukio ya ukiukwaji wa haki za binadamu, wakati akiwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Mwanaharakati Fatma Karume, amechambua uteuzi huo akiandika “kama huyu ndiye tumaini ya CCM, nakuombeni kwa heshima na taadhima mfikirie upya mikakati yenu. Kweli kwenye watu milioni 60 Paulo ndiye tumaini la CCM? Mnaharibu nchi yetu.”

“Ukiona propaganda za kusifu maamuzi zinaanza, elewa kuwa wameshatambua uamuzi haukuwa sahihi, sasa wanajaribu kuisafisha. Mlitegemea kumrejesha Paulo itakuwa Popular? Huyu aliwatukana wabunge wa CCM sembuse sisi wananchi au mmesahau?” ameandika Fatma

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Biteko: Samia ni muumini wa maridhiano sio kwa kuigiza

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Mpango: Sitakufa bali nitaishi

Spread the loveMAKAMU  wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk....

Habari za SiasaTangulizi

Mbowe: Miaka 62 ya uhuru tujenge upya mioyo yetu

Spread the loveWAKATI Tanganyika ikiadhimisha miaka 62 tangu kupata uhuru, Mwenyekiti wa...

Habari za Siasa

Rais Samia asamehe wafungwa 2,244

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amewasamehe wafungwa 2,244, huku akiwabadilishia...

error: Content is protected !!