Sunday , 28 April 2024
Habari za SiasaTangulizi

Makonda amvaa Lissu

Spread the love

KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Paul Makonda, amesema kuna shuthuma nyingi zinaelekezwa kwake, lakini ameamua kukaa kimya kwa kuwa anaheshimu maono ya Rais Samia Suluhu Hassan, yanayoelekeza watu kuvumiliana. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Makonda ametoa kauli hiyo leo tarehe 5 Machi 2024, akizungumzia tuhuma zinazotolewa na baadhi ya watu juu yake, huku akimnyooshea kidole Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Bara, Tundu Lissu, akidai amekuwa akimhukumu bila kumpa nafasi ya kumsikiliza.

“Nimeona vitu vingi sana, nimemuona mwanasheria wetu kaka yangu Tundu Lissu anaongea vitu yaani kinyume na taaluma, yaani huwezi kujua kama ni mwanasheria aliyesomea sheria lakini bahati nzuri amepata umaarufu basi akikaa kwenye kipaza sauti anasikilizwa. Lakini wanasema kumhukumu mtu ambaye hujawahi kupata nafasi ya kumsikiliza,” amesema Makonda.

Makonda amesema “sasa mwanasheria anasimama anatoa hukumu kwa watu na kuwapa hatia wakati ukiuliza hivi… nimesikia. Sasa wewe mwanasheria unaishi kwa kusikia, umeskia wapi upande mmoja ni kinyume na taaluma.”

Mwenezi huyo wa CCM amedai kuwa, hamjibu Lissu kwa kuwa anajua kwamba kuna changamoto anazopitia kama mtu mzima.

“Najua kaka yangu Lissu kuna changamoto anazopitia na kama mtu mzima lazima utambue mwenzake shida anazopitia na unaelewa. Kwa hiyo wale wote wanaosema na kubaki kunishambulia binafsi wanasahau kazi yangu. Ukiwachunguza unajua huyu ana changamoto hii anayopitia na hali ndivyo ilivyo tunavumiliana na rais wetu ametufundisha tuwe na uwezo mkubwa wa kuvumiliana kwa hii ndiyo maana hutasikia mimi nahangaika kubishana nao,” amesema Makonda.

Licha ya Makonda kutotaja tuhuma ambazo Lissu anazielekeza kwake, makamu mwenyekiti huyo wa Chadema mara kadhaa amemtuhumu kuhusika katika tukio la kushambuliwa risasi na watu wasiojulikana Septemba 2017 jijini Dodoma.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde aibana kampuni kutimiza masharti ya mkataba

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameitaka Kampuni ya Xin Tai...

Habari za Siasa

Sauti ya Watanzania waeleza sababu za kuiunga mkono Chadema

Spread the love  KIKUNDI kinachojipambanua katika kupigania rasilimali na uhuru wa nchi,...

Habari MchanganyikoTangulizi

Jacob, Malisa waachiwa kwa masharti

Spread the love  JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

error: Content is protected !!