Saturday , 27 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Makaburi ‘yatoweka’ kinyemela Segerea
Habari Mchanganyiko

Makaburi ‘yatoweka’ kinyemela Segerea

Spread the love

 

MKAZI wa Kinyerezi, jijini Dar es Salaam, aliyefahamika kwa jina moja la Sakina, ameangua kilio akitaka aoneshwe yalipo mabaki ya mwili wa mjukuu wake, Esther Alphonce, anayedaiwa kuzikwa kwenye makaburi ya Zimbili, kata ya Kinyerezi wilayani Ilala. Anaripoti Mary Victor … (endelea).

Esther anayedaiwa kuzikwa kwenye makaburi hayo tarehe 8 Agosti 2014 akiwa na umri wa miezi miwili, mpaka sasa kaburi lake halijulikani halipo baada ya taarifa kudai lilifukuliwa na eneo hilo kuzikwa mtu mwingine.

Akiwa kwenye makaburi hayo kujionea hali halisi, Sakina alisema “migogoro hii ni ya muda mrefu mpaka kikaletwa kibao cha kuzuia watu kuzikwa kutokana na eneo hilo kuonekana limejaa.”

“Pamoja na tangazo hilo, lakini watu wameendelea kuzikwa, ninalotaka kufahamu mabaki ya mjukuu wangu waliyaweka wapi, maana uongozi wa zamani ulifanyiwa kazi kwa kuweka kibao lakini bado agizo hilo linakiukwa, ninachohitaji ni mabaki ya mjukuu wangu nikayahifadhi.

“Kufukua miili iliyozikwa inafahamika na lilishakutwa fuvu pale juu ya kaburi, watu, majirani walishalia sana, naona suala limekuwa endelevu kwa hiyo huu ni unyanyasaji wa kiwango cha juu, wanafukua makaburi, wanachukua misalaba wanaifuta majina na kuiuza tena.”

Mama mzazi wa Esther aitwaye Anitha Joseph, alisema kaburi la mtoto wake limefukuliwa na kuzikwa mtu mwingine.

“Nimelijua hilo baada ya kwenda kutembelea kaburi lake na kukutwa amezikwa mtu mwingine,” alisema

“Nilipowauliza wale wanaofanya uchimbaji na kutoa huduma makaburini hapo, hawakuwa na majibu yoyote,” alisema Anitha.

Mkazi jirani na makaburi hayo, aliyetaka hifadhi ya jina lake alisema si tu kufukua miili, bali wamefikia hata kuchimba ndani ya viwanja vya watu.

“Mwenye kiwanja alipopewa taarifa kwamba kiwanja chake kinachimbwa kaburi, alipiga simu na kutaka wachimbaji waondoe kaburi hilo maana walishaanza kulijengea. Kero hii ni ya muda mrefu sana. Kila watu wakija hawaoni makaburi walipohifadhi ndugu zao na kujikuta wakiangua vilio,” alisema mkazi huyo.

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Zimbili, Hassan Nandeta alisema:”Kuna mama aliwahi kuja kulalamika na niliahidi kufanyia kazi malalamiko yake. Hata hivyo, uongozi wa serikali ya mtaa uliomaliza muda wake, uliwauzia watu baadhi ya vipande makaburini hapa.

“Hilo lilifanyika baada ya kujaa kwa makaburi ya Ukonga na ya Segerea, hivyo wengi wao wakatamani kuja kununua maeneo huku ili wahifadhiwe jirani na walikohifadhiwa jamaa zao, kwa mfano mama, baba, ndugu wa karibu. Kwa hiyo yapo maeneo yanayomilikiwa na baadhi ya watu.

“Hata hivyo, makaburi yanayolalamikiwa kufukuliwa ni ambayo hayakujengewa wala kuwekewa mashahidi (alama),” alisema Nandeta.

Hivi karibuni kuhusu Diwani wa Kinyerezi, Leah Leonard akizungumzia malalamiko hayo alisema: “Aisee! Hayajanifikia, sijawahi kupewa malalamiko na wananchi wangu.

“Kabla ya hawajafika huko, sidhani kama walifika ngazi ya mtaa. Lakini kwenye ofisi yangu malalamiko hayo hayajafika, ila nashukuru kwa taarifa, nami nitakualika katika kata yangu,” alisema Leah.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!