Sunday , 5 February 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko MeTL yarekebisha Bajaj kuboresha mapato
Habari Mchanganyiko

MeTL yarekebisha Bajaj kuboresha mapato

Mmoja wa wamiliki bajaji, Juma Ahmadi
Spread the love

 

KAMPUNI ya Mohammed Enterprises Ltd (MeTL) imeamua kurejesha fadhila kwa wateja wake kwa kutoa huduma za kurekebisha (services) bajaji zaidi ya 1,500 ili kuboresha mapato kwa vijana nchini. Anaripoti Christina Haule, Morogoro … (endelea).

Mwakilishi wa MeTL, Zakayo Edward ambaye pia ni muuzaji wa Bajaj hizo nchini Tanzania na Afrika kwa ujumla alisema hiyo ni sehemu ya uwajibikaji wa kijamii kwa Jamii (CSR) unaofanywa na MeTL, na kwamba katika utafiti mdogo waliofanya wamebaini kuwa madereva wengi wa Bajaji hawafikirii hali ya vyombo vyao na kuzifanyia huduma (services) kwa wakati.

“Ni lengo la Mohammed kupitia CSR, tutatoa huduma kwa Bajaji 1,500 kote nchini, ambazo ni RE4s na Maxima ili kuzipa ubora na kuzalisha mapato ya vijana wa Kitanzania wanaokabiliwa na changamoto ya ukosefu wa ajira,” alisema.

Alitaja idadi ya Bajaji ambazo tayari zimepatiwa huduma ni pamoja na mkoa wa Iringa 200, Dodoma 250 wakati 500 katika ukanda wa ziwa pamoja na jiji la Mwanza, Sengerema na Geita, Kigoma 150, Morogoro 150, Arusha 150, Dar es Salaam 300 na Kilimanjaro 200.

Aidha Edward aliwashauri wamiliki wa Bajaji kutumia mafuta ya Idemitsu 20w50 na kuhakikisha wanafuata kanuni za kubadilisha mafuta kila baada ya wiki mbili huku wakiondoa baadhi ya vifaa vilivyochoka na kuweka vipya ili kufanya bajaj kuendelea kuwa na uwezo wake.

Alisema hivi karibuni kampuni hiyo itatoa bajaji zenye ubora zaidi ya zilizopo, ambazo zitakuwa na redio na mnara wa kusoma matumizi ya mafuta na mwendo sambamba na ubora wake kwa kuwa na injini inayoendesha kilomita 4,000 kwa mafuta kidogo.

Naye Afisa masoko wa ukanda wa kati, Kenny Mwangosi ametoa wito kwa wamiliki kuzingatia aina ya Bajaji na asili ya barabara ili kuzifanya bajaji zao kubaki katika ubora wake katika muda uliopangwa kwa matumizi.

Alisema bajaj aina ya Maxima ina malengo mengi kwani inachukua abiria 7 huku ikiwa na injini yenye nguvu hata ya kupandisha kwenye milima wakati RE4s inachukua abiria 4 huku ikiwa na uwezo mzuri wa kutembea maeneo tambarale zaidi.

“Ingawa wengi wanapendelea RE4s kwa sababu ya matumizi ya mafuta lakini huchukua abiria wachache kuliko Maxima na hivi karibuni kampuni itasambaza Bajaji ya kisasa ambayo inafuta udhaifu wote wa bidhaa mbili,” alisema.

Awali mmoja wa wamiliki wa bajaji, Juma Ahmad, ambaye pia ni dereva wa bajaji zinazofanya safari mjini, aliimshukuru kampuni ya MeTL kwa CSR kwa sababu mbali na kutoa huduma, wamefanikiwa kuelimika na kuona umuhimu wa huduma kwa wakati katika bajaji zao.

Alisema wameelimika na kujua kuwa suala la umwagaji mafuta kila baada ya wiki mbili linapaswa kuenda sambamba na kuondoa vifaa vilivyochoka ili kuboresha mfumo mzima wa bajaji.

Aidha alisema kutokana na msaada wa kubadilishiwa mafuta na matengenezo madomadogo waliyopata kwa bajaji zaidi ya 100 Manispaa ya Morogoro, wanaweza kufanya biashara na kuwekeza mitaji baada ya kukidhi mahitaji yao hasa pale serikali itakapowapanga kwenye vituo vyenye wateja wa kutosha.

 

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Haya hapa majina 12 ya familia moja waliofariki kwenye ajali Tanga

Spread the love  MAJINA 12 kati ya 17 ya waliofariki dunia katika...

Habari Mchanganyiko

Rais Samia awalilia 17 waliofariki ajalini wakisafirisha maiti

Spread the love  RAIS Samia Suluhu Hassan, ametuma salamu za rambirambi kwa...

Habari Mchanganyiko

Wanawake wachimbaji wajenga zahanati kuokoa afya za wakazi 2000

Spread the love  ZAIDI wakazi 2,000 wa kijiji cha Nyamishiga Kata ya...

Habari Mchanganyiko

Baada ya Congo DR, Somalia mbioni kujiunga na EAC

Spread the love  TAIFA la Somalia liko mbioni kuwa mwanachama rasmi wa...

error: Content is protected !!