September 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Majina waliochaguliwa kujiunga Kidato cha Kwanza haya hapa

Wanafunzi wa darasa la saba wakifanya mtihani

Spread the love

BARAZA la Mitihani nchini (NECTA), limetangaza majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Kwanza nchini. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma…(endelea).

Akitangaza majina hayo leo tarehe 5 Desemba 2019, Selemani Jafo, Waziri wa Ncho, Ofisi ya Rais –Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) amesema, asilimia 92.27 ya wanafunzi waliofanya mtihani wa Darasa la Saba mwaka huu, wamechaguliwa kujiunga na Kidato cha Kwanza mwakani.

Amesema, asilimia hiyo inaakisi jumla ya wanafunzi 701,038 kwamba ndio waliochaguliwa.

Amesema, wanafunzi 58,699 wameshindwa kuchaguliwa kutokana na kukosa madarasa huku Mkoa wa Kigoma, ukiwa na kiwango kikubwa cha upungufu huo. Wanafunzi 909 ndio waliofutiwa matokeo kutokana na udanganyifu.

Amesema, katika wale waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Kwanza, wavulana ni 335, 513 na wasichana ni 365, 525.

Angalia majina ya wanafunzi wa darasa la saba na shule wanazoenda hapa.

error: Content is protected !!