Friday , 26 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Majaliwa: LNG mbioni kuanza kuzalishwa
Habari Mchanganyiko

Majaliwa: LNG mbioni kuanza kuzalishwa

Spread the love

 

WAZIRI Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema, Serikali ipo mbioni kuanza kutekeleza mradi wa kimkakati wa uzalishaji wa gesi asilia ya kimiminika (LNG) mkoani Lindi, utakaogharimu dola za kimarekani bilioni 30. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Amesema kuwa mradi huo ni moja ya mradi wa kimkakati ambao Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amepania kuutekeleza katika awamu ya sita ambao utakapoanza kutekelezwa utatumika kwa kipindi cha zaidi ya miaka 25.

Ametoa kauli hiyo jana Jumamosi tarehe 5 Juni 2021, wakati wa mkutano na wadau wa maendeleo wa wilaya ya Lindi, katika ukumbi wa hoteli ya Sea View Mjini Lindi.

“Vile viwanja mlivyovichukua anzeni kuvijenga, mradi wa gesi asilia unakuja, nina amini mradi huu ukianza baada ya kukamilisha makubaliano, tutafika hatua nzuri” alisema.

Aidha, Majaliwa alizitaka Halmashauri nchini, ziongeze usimamizi kwenye sekta ambazo wananchi wanazitekeleza kila siku ikiwemo sekta ya kilimo na kuifanya moja ya agenda muhimu kwa kuwa watanzania wengi wanategemea kilimo katika kujipatia kipato.

“Halmashauri zetu nyingi watu wake ni wakulima, wafanyakazi ni asilimia tano tu na hata wafanyabishara ni asilimia ndogo, viongozi simamieni kilimo ili kiimarishe mapato ya mtu mmoja mmoja,” alisema

Pia, Waziri Mkuu aliwataka wananchi wa Lindi kufanya kazi kwa bidii na weledi ili kuinua uchumi wa mkoa huo na taifa kwa ujumla, “tutumie fursa zilizopo ndani ya mkoa kuhakikisha uchumi wetu unapanda, kila mtu afanye kazi katika eneo lake.”

Vilevile, Waziri Mkuu alisema, ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya 2020/25 inaelekeza kuwa katika kujenga uchumi ni lazima uakisi maisha halisi ya kila siku ya wananchi na uwe uchumi shirikishi na shindani.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Zainabu Telack alisema, watahakikisha rasilimali zilizopo mkoani humo zinawanufaisha Wana-Lindi na Taifa kwa ujumla.

“Tumekubaliana kwamba lindi ni tajiri, biashara zote zinazofanyika kwasasa tunakwenda kuzitafsiri katika maisha ya watu wetu,” alisema

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!