July 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Uchaguzi mkuu TFF Agosti 8

Ofisi za TFF

Spread the love

 

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limetangaza Uchaguzi Mkuu wa shirikisho hilo, utafanyika tarehe 7 Agosti 2021. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Taarifa iliyotolewa leo Jumapili, tarehe 6 Juni 2021 na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi wa TFF, Wakili Kiomoni Kibamba amesema, nafasi zitakazowaniwa ni ya urais na wajumbe sita wa kamati tendaji.

Wakili Kibamba amesema, fomu za kuwania nafasi hizo zitaanza kutolewa Jumanne ya tarehe 8 hadi 12 Juni 2021, ofisi za TFF na tovuti ya shirikisho hilo.

Amesema, gharama ni Sh.500,000 kwa nafasi ya urais na Sh.200,000 kwa wajumbe wa kamati tendaji.

Kwa sasa, Rais wa TFF ni Wallence Karia ambaye amewahi kusema, atawania tena nafasi hiyo katika uchaguzi mkuu ujao.

error: Content is protected !!