December 1, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Majaliwa atoa maagizo kwa Waziri Jafo, bosi NSSF

Spread the love

 

WAZIRI Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amemuagiza Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Seleman Jafo kukamilisha andiko ili kuzuia matumizi ya kamba za plastiki. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo jana Alhamisi, tarehe 18 Novemba 2021, alipotembelea kiwanda hicho ambacho kabla ya kufanyiwa maboresho kilikuwa kinazalisha tani 1.5 hadi 2.5 kwa siku ambapo kwa sasa kinazalisha tani 20 kwa siku.

“Leo tunalima mkonge, hapa Tanga mnalima mkonge na zinazalisha kamba za katani, kamba Tanzania ni nyingi, likishatoka tangazo hakutakuwa na ruhusa ya kutumia kamba za plastiki nchini,” alisema

Aidha, Majaliwa amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Masha Mshomba atoe kipaumbele kwa wakazi wa eneo la Ngomeni katika suala la ajira kwenye kiwanda cha kuzalisha bidhaa zinazotokana na zao la mkonge cha Sisalana.

NSSF ilitoa takribani Sh.2.5 bilioni kwa ajili ya kukifufua ikiwa ni utekezaji wa kampeni ya ujenzi wa viwanda katika kiwanda hicho kilichoko katika eneo la Ngomeni Mkoani Tanga ambacho

Majaliwa amesema kwa kuwa kiwanda hicho ambacho kipo katika kata ya Ngomeni wilayani Muheza ni vema kwa uongozi wa NSSF ukatoa kipaumbele cha ajira kwa wananchi wanaozunguka eneo ili waweze kunufaika na uwepo wake.

Kwa upande wake, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Uratibu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama amewaagiza Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, mkurugenzi mkuu wa NSSF pamoja na Afisa Kazi wa Mkoa wa Tanga wakutane na waliokuwa wafanyakazi wa kiwanda hicho na kushirikiana nao kutatua changamoto zinazowakabili.

Kampuni ya Sisalana ilianza kazi rasmi kiwandani tarehe 12 Machi 2021, ambapo ilikuta hali ya uzalishaji ikiwa ni ya kusuasua kutokana na ukosefu wa mtaji wa kuendeshea biashara na uchakavu wa mitambo.

error: Content is protected !!