December 1, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mgao wa maji, umeme Tanzania: Ni mwendo wa matamko

Spread the love

 

MJADALA juu ya mgawo wa umeme na uhaba wa maji, umeiweka Serikali ya Tanzania njia panda, baada ya baadhi ya viongozi wake wakuu, kutoa kauli zinazokinzana. Anaripoti Gabriel Mushi, Dar es Salaam … (endelea).

Akizungumza Mwanza jana Alhamisi, tarehe 18 Novemba 2021, kwenye maadhimisho ya Jubilei ya Miaka 50 ya Hospitali ya Rufaa ya Bugando, Rais Samia Suluhu Hassan alisema, mojawapo ya sababu za uhaba wa maji hata kusababisha mgawo na upungufu wa umeme, “ni hujuma za makusudi, zinazofanywa na baadhi ya watu wanaozunguka Mto Ruvu.”

Alisema, watu wamejenga vizuizi, Mto Ruvu, hali inayoashiria uhujumu wa masukudi wa kuzuia maji kwenda kwenye mitambo ya Ruvu Chini na Ruvu Juu, jambo ambalo linasababisha uhaba wa maji, Dar es Salaam na Pwani.

Aidha, Rais Samia alisema, operesheni ya kuangalia chanzo cha uhaba wa maji katika Mto Ruvu, imebaini kuwapo watu waliochepusha maji ili yaende kwenye kilimo na matumizi mengine.

Aliutoa kauli hiyo, taribani wiki tatu sasa, baada ya kuwapo mgawo wa kimyakimya wa umeme, hatua ambayo ilimfanya Spika wa Bunge, Job Ndugai, kuagiza Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati, kushughulikia jambo hilo.

Undani wa habari hii na kujua kauli kinzani za viongozi, soma Gazeti la Raia Mwema, toleo la leo Ijumaa 19 Novemba 2021

error: Content is protected !!