Saturday , 27 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Majaliwa atoa maagizo kwa DC, Madiwani Kaliua
Habari Mchanganyiko

Majaliwa atoa maagizo kwa DC, Madiwani Kaliua

Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu wa Tanzania
Spread the love

 

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa ameagiza ujenzi wa kituo cha Afya Usinge, wilayani Kaliua, Mkoa wa Tabora, ukamilike ifikapo Oktoba 2021. Anaripoti Mwandishi Wetu, Tabora…(endelea).

Waziri Majaliwa ametoa agizo jana tarehe 28 Agosti 2021, baada ya kutembelea ujenzi wa kituo hicho na kukuta umekwama,tofauti na maelezo aliyopatiwa awali.

Waziri Majaliwa alitoa agizo hilo, baada ya kubaini alipewa taarifa za uongo juu ya ujenzi wa kituo hicho.

Ambapo alielezwa kwamba fedha Sh. 600 milioni, zilizotolewa kwa ajili ya ujenzi wa kituo hicho, sehemu yake zilitumika kununua vifaa vya ujenzi, lakini alipofika kukagua ujenzi huo, hakuvikuta vifaa hifaa hivyo.

Kufuatia changamoto hiyo, Waziri Majaliwa, amemuagiza Mkuu wa Wilaya (DC) ya Kaliua, mkoani Tabora, Paul Matiko, kusimamia ujenzi wa kituo hicho na kuhakikisha kinakamilika ili wananchi wa maeneo hayo waweze kupata huduma za afya.

“Sitawaelewa mkiniambia mnatafuta fedha nyingine na kuzileta hapa ili muongeze kwenye milioni 620 kukamilisha ujenzi wa majengo katika kituo hiki, na hili watu mjiande, Serikali yetu ipo makini na usimamizi wa fedha za serikali upo vilevile,” alisema Waziri Majaliwa.

Aidha, Waziri Majaliwa aliwaagiza madiwani wa eneo hilo, kusimamia fedha zinazotolewa na Serikali kwa ajili ya kuboresha huduma za afya.

“Mheshimiwa Rais, ameleta kwenye Wilaya yenu Sh. 1,860,000,000 bilioni kwa ajili ya dawa na kila mwezi halmashauri inapokea fedha Sh. 165 milioni. Mna vituo vya afya na zahanati, nisisikie vituo hivyo vinakosa dawa. Madiwani naomba msimamie katika vituo hivyo kusiwe na mapungufu,” alisema Majaliwa.

Katika Hatua nyingine, Waziri Majaliwa aliiagiza Wizara ya Maliasili na Utalii, kupitia Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), iyapige mnada magogo yaliyokamatwa baada ya kukatwa kwa njia haramu.

“Wizara toeni vibali vya mnada magogo haya yauzwe na yaliyo humo ndani hifadhini, TFS nendeni mkayakusanye haraka sana ili mpaka mwishoni mwa Septemba yawe yamekusanywa na kuuzwa kupitia mnada, waambieni wanunuzi mtayapiga mnada lini ili waje hapa kila mtu ajaribu bahati yake,” alisema Waziri Majaliwa.

Aidha, Waziri Mkuu ameagiza Mamlaka ya Usimamizi Wanyamapori Tanzania (TAWA), kuongeza ulinzi katika eneo la hifadhi hiyo, ili kuwalinda wanyama wanaokatiza na wasisite kuwachukulia hatua kali wale watakaokamatwa wakifanya ujangili.

“Hawa lazima tuwafanyie msako tuwakamate, awe anatoka Tanzania au nje ya nchi, ana silaha, kamata aingie kwenye mkono wa sheria, tengeneza timu yako upekuzi ufanyike,” alisema Waziri Majliwa.

Akiongea na Wanakijiji cha Wachawaseme, wilayani humo, Waziri Majaliwa amewasihi kuulinda msitu ulio katika pori la akiba la Igombe kwa kuacha kukata miti ili kulinda uoto katika eneo hilo.

“Tunaharibu miti, hili bonde lote ni eneo linalosaidia kutoa maji kwenda mto Malagarasi lakini pia ziwa Tanganyika, mkiacha miti iondolewe eneo hili litakuwa kavu na hakutakuwa na maji, hapa ni nyumbani kwenu, ni wajibu wenu kulinda maliasili hii,” alisema Waziri Majaliwa.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!