Friday , 3 February 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Wapinzani wataka IGP Sirro ajiuzulu
Habari za Siasa

Wapinzani wataka IGP Sirro ajiuzulu

IGP, Simon Sirro
Spread the love

 

VYAMA vya Upinzani nchini Tanzania, vimelaani kauli ya Inspekta Jenerali wa Polisi nchini humo, IGP Simon Sirro, dhidi ya familia ya Hamza Mohammed, aliyewauwa Askari Polisi watatu na mlinzi mmoja wa Kampuni ya Ulinzi ya SGA. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Jana Jumamosi, tarehe 28 Agosti 2021, akizungumza na wanahabari mkoani Dar es Salaam, IGP Sirro aliihoji familia ya Hamza, inajisikiaje baada ya kijana wao kufanya mauaji hayo Jumatano iliyopita, maeneo ya Ubalozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Kinondoni mkoani humo.

Leo tarehe 29 Agosti 2021, ACT-Wazalendo kupitia kwa Naibu Katibu wake wa Habari, Unenezi na Mahusiano na Umma, Janeth Rithe, kimesema kauli hiyo imekosa weledi.

“Matamshi ya IGP Sirro ni kielelezo cha kukosa weledi, ni jambo la kusikitisha kuwa mtu wa ngazi ya IGP anashindwa kufahamu kuwa, hulka ya jinai ni suala la mtu binafsi na wala si la uzawa wala la familia ya mtu,’ imesema taarifa ya Rithe.

Taarifa ya Rithe imesema, IGP Sirro anapaswa kujiuzulu au mamlaka iliyomteua imuwajibishe kufuatia kauli hiyo.

“IGP Sirro ajiuzulu, ni dhahidi kuwa hana sifa ya kuliongoza Jeshi la Polisi, lenye weledi kwa karne ya 21, kazi imemshinda, kachoka, tunamtaka ajiuzulu la sivyo mamlaka yake ya uteuzi imwajibishe,” imesema taarifa ya Rithe.

Nacho Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kupitia ukurasa wake wa Twitter, kimeiomba mamlaka iliyomteua IGP Sirro imuwajibishe, kwa madai kuwa kauli yake inaweza leta mgogoro.
“Kauli za IGP Sirro zinafaa kulaaniwa na kukemewa kwa nguvu zote, kwani zinaashiria shari na uchochezi wa vurugu nchini. Mamlaka ya uteuzi imchukulie hatua sasa kabla hajalitumbukiza Taifa kwenye mgogoro,” imesema taarifa ya Chadema.

Askari Polisi waliopoteza maisha katika tukio hilo ni, Miraji Khatib Tsingay, Emmanuel Keralya na Kangae Jackson.Mlinzi aliyefariki ni Joseph Okotya Mpondo.

Baada ya Hamza kufanya mauaji hayo, aliuawa wakati akijibizana kwa risasi na Polisi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Vijana ACT-Wazalendo Dar wampa tano Rais Samia

Spread the love  NGOME ya Vijana ya Chama cha ACT-Wazalendo, kimempongeza Rais...

Habari za Siasa

ACT-Wazalendo yaiangukia Serikali kunusuru wananchi Liwale, Nachingwea

Spread the love  CHAMA cha ACT-Wazalendo, kimeitaka Serikali kuchukua hatua za haraka...

Habari za SiasaTangulizi

Vigogo wanaokwamisha mradi Liganga na Mchuchuma kitanzani

Spread the love  NAIBU Spika wa Bunge, Mussa Zungu, watu wanaokwamisha utekelezaji...

Habari za Siasa

Gridi ya Taifa kufumuliwa kukabiliana na katizo la mgao wa umeme

Spread the love  WAZIRI wa Nishati, Januari Makamba, amesema Serikali ina mpango...

error: Content is protected !!