Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Habari Majaliwa aipongeza Yanga kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu
HabariMichezoTangulizi

Majaliwa aipongeza Yanga kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu

Spread the love

 

WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa, ameipongeza klabu ya soka ya Yanga kwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2021/22. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Majliwa amewap[ongeza mabingwa hao Bungeni jijini Dodoma, wakati akitoa hotuba ya kufunga mkutano wa saba kikoa cha 55.

Waziri Mkuu huyo ambaye ni mdau mkubwa wa michezo aliwapongeza mabingwa hao kwa kusema kuwa, timu hiyo ilikuwa na msimu mzuri toka kuanza kwa Ligi na hivyo walistaili kutwaa taji hilo.

“Nichukue nafasi hii kuwapongeza Yanga (Wananchi) kwa kuibuka vinara wa Ligi Kuu ya NBC, hongereni sana mlikuwa na msimu mzuri na mlistaili kuwa Mabingwa.” Alisema Majaliwa

Yanga imetwaa ubingwa wa Ligi Kuu mara baada ya kuukosa katika kipindi cha miaka minne, huku wakiingia kwenye rekodi ya kutwaa ubingwa huo bila kupoteza mchezo wowote.

Katika msimu huu, Yanga imecheza michezo 30 ya Ligi huku kati ya hiyo ikifanikiwa kuibuka na ushindi katika michezo 22, na kwenda sare mara nane.

Ubingwa huo utaifanya Yanga kuiwakilisha nchi katika michuano ya klabu bingwa Barani Afrika, kwa msimu ujao wa mashindano 2022/23, sambamba na klabu ya Simba ambayo imeshika nafasi ya pili na itakwenda kwenye michuano hiyo kufuatia Tanzania kupata uwakilishi wa timu nne.

Aidha katika hatua nyingine Majaliwa aliwapongeza pia, Timu ya taifa ya wasichana chini ya umri wa miaka 17 (Serengeti Girls), kwa kufanikiwa kufuzu kwa fainali za kombe la Dunia kwa wasichana zinazotarajia kufanyika Oktoba mwaka huu, nchini India.

“Lakini pia napenda kuipongeza Timu ya Serengeti Girls kwa kufuzu kombe la Dunia mwaka huu India, na kukamilisha idadi ya timu 16 zitakazoshiriki faiali hizo.” Aliongezea Waziri Mkuu

Katika fainali hizo Serengeti Girls tayari imepangwa kundi D, sambamba na timu za Taifa za Ufaransa, Canada na Japan.

https://www.youtube.com/watch?v=x3pl5A08Lng

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Michezo

EPL, Ligue 1 na Coppa Italia kinawaka leo

Spread the love  LEO ligi kadhaa zitaendelea nchini barani ulaya ikiwemo ligi...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

BiasharaMichezo

NBC yaunga mkono jitihada kutokomeza malaria

Spread the loveKuelekea Maadhimisho ya siku ya malaria Duniani yatakayofanyika kesho Aprili...

error: Content is protected !!