August 19, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wataalam wa afya watakiwa kutumia weledi

Spread the love

 

WATAALAMU wa Afya Nchini Tanzania, wameshauriliwa kufanya kazi kwa kuzingatia weledi, uadilifu na maadili ya taaluma yao kwa kutunza miundominu ya majengo yaliyojengwa na rasilimali zinazonunuliwa. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea)

Mkurugenzi Msaidizi wa Afya-Tamisemi, Dk. Paul Chaote ametoa kauli hiyo Dodoma wakati akifungua kikao kazi cha siku tatu kwa waratibu wa maabara na wafamasi wa mikoa nchini.

Dk Chaote amesema , watalaamu hao wanatakiwa kutunza miundombonu na rasilimali ili ziendelee kuwa katika hali ya ubora kwa muda mrefu na kuendelea kusaidia katika utoaji wa huduma ya afya.

“Hivyo ni vizuri kila mmoja akatimize wajibu wake kikamilifu katika kutunza miundombinu na rasilimali,” amesema .

Dk Chaote alihimiza uwajibikaji katika maeneo yao ya kazi ili kuwezesha kuboresha huduma za afya kwa wananchi.

Dk. Chaote amesema serikali kwa upande wake, inatambua kuwa katika kuyafikia Malengo Endelevu ya Maendeleo, afya ni moja ya mhimili muhimu katika kuwezesha kufikiwa malengo hayo. Hivyo, bila uwajibikaji hawataweza kufikia malengo hayo.

Amesema Ofisi ya Rais-Tamisemi inazisisiza watalaamu na wadau wote wanatakiwa kusimamia kutolewa kwa huduma bora kwa wananchi kwa kutatua changamoto zinazikibali sekta ya afya katika eneo husika.

Waratibu hao wa mikoa wanatakiwa kuimarisha mkakati wa kusimamia afua zilizopangwa ili kufikia malengo husika.

Pia amehimiza Timu za Usimamizi wa Huduma za Afya ngazi ya mkoa (RHMT) na za Halmashauri (CHMT) kufanya usimamizi shiriki katika vituo vya kutolea huduma za safya mara kwa mara.

Dk Chaote amesema wanatakiwa kufanya usimamizi wenye tija na ili kupata matokeo chanya.

Dk Chaote amesema katika mwaka wa fedha 2021/22, Ofisi ya Rais-Tamisemi ilidhinishwa Sh bilioni 11.30 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa na vifaa tiba kwa ajili ya hospitali 31 za awamu ya pili ziliazonanza kujengwa mwaka 2018/19.

Aidha hadi mwaka 2021, OR-Tamisemi ilipeleka Bohari ya Dawa (MSD) Sh bilioni 98 kwa ajili ya ununuzi na usambazaji wa vifaa katika vituo vilivyoboreshwa.

Lakini pia, kupitia mpango wa IMF, Serikali ilinunua vifaa tiba vyenye thamani ya Sh bilioni 94.4 ambavyo baadhi ya vifaa hivyo vinatoa huduma kwenye majengo ya dharura na wagonjwa mahututi yaliyojengwa hivi karibuni.

Hivyo basi, aliwataka wafamasia na watalaamu wa maabara kwenda kusimamia vifaa hivyo ipasavyo na kuhakikisha vinatoa huduma iliyokusudiwa.

“Ni nia ya serikali kuhakikisha kuwa mwananchi wanapata huduma ya afya iliyobora na karibu ya maeneo anayoishi.

Amesema serikali imeendelea kutoa ajira kwa watumishi katika mamlaka za serikali za mtaa, madhalani katika mwaka wa fedha 2021/22, serikali kupitia mejenejimenti ya utumishi wa umma imetoa vibali vya nafasi za ajira 7,612 za watumishi wa kada ya afya pamoja na watalaamu wa radiolojia.

Pamoja na jitihada hizo za serikali, bado katika eneo la uwajibikaji wa watumishi mmoja mkoa katika maeneo ya kazi bado hawajatenda haki.

Awali akizungumza Mwakilishi wa Wadau katika Mnyororo wa Thamani, Bwiro Magesa amesema kwamba wafanyakazi wanatakiwa kujituma.

Naye Msajili wa Bodi ya Maabara Binafsi, Dominic Fwiling’afu alisema waratibu hao wa mikoa kuwajibika kikamilifu katika utendaji wa kazi zao.

Naye Msajili wa Baraza la Famasia, Elizabeth Shikalage aliwataka wafamasia hao na watalaamu wa maabara kutenganisha kazi zao kwani imekuwa ni kawaida kuona kwenye maabara dawa zinauzwa na kwenye famasi wanapimwa vipimo.

error: Content is protected !!