Thursday , 28 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Uhuru wa uhariri wa habari unaingiliwa – Wakili Marenga
Habari Mchanganyiko

Uhuru wa uhariri wa habari unaingiliwa – Wakili Marenga

James Marenga, Makamu Mwenyekiti MISATAN
Spread the love

 

HATUA ya mhariri wa chombo cha habari kuelekezwa na serikali taarifa za kuchapisha, kama ilivyolekezwa na kifungu cha cha 7 (2) (b) cha sheria hiyo, inaingilia moja kwa moja uhuru wa mhariri katika kutoa ama kuchapisha habari. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Hayo yameelezwa na Makamu Mwenyekiti wa MISA – TAN, Wakili James Marenga, katika semina kwa wanahabari iliyofanyika leo Alhamisi tarehe 30 juni 2022 jijini Dar es Salaam.

Marega amesema kifungu hicho cha sheria kinapoka mamlaka ya mhariri katika kuamua habari gani ya kuchapishwa.

“Kifungu cha 7 (2) (b) (iv) cha Sheria ya Huduma za Habari, kinatoa maelekezo kwa vyombo vya habari binafsi kuchapisha habari zenye umuhimu kwa taifa kwa maelekezo ya Serikali.

Kifungu hiki cha Sheria kinaingilia uhuru wa uhariri na hasa kwenye vyombo vya habari vya binafsi. Kifungu hiki kidogo hakiwezi kufanyiwa marekebisho, tunapendekeza kifutwe,” amesema.

Amesema, mapendekezo yanakusudia kuwezesha maamuzi ya kihariri kuzingatia vigezo vya taaluma bila kuathiriwa na maamrisho yasiyo ya kitaaluma. Uhuru wa uhariri (editorial independence) utalindwa.

Akifafanua zaidi amesema, kifungu cha 7 (3), (a), (b), (c), (f), (g), (h), (i) na (j) vya Sheria hiyo, vinatoa udhibiti wa aina fulani ya habari ama maudhui.

“Mamlaka hii ya kisheria inatoa mwanya kwa serikali kudhibiti taarifa zinazotolewa na vyombo binafsi vya habari.

“Kifungu hiki na vifungu vyake vidogo vinakiuka uhuru wa wa kujieleza bila ya kuwa na sababu za msingi. Hii pia ni kwa mujibu wa maamuzi ya Mahakama ya Haki ya Afrika ya Mashariki (EACJ).

Amesema, tunapendekeza kifungu hiki na vifungu vyake vidogo vifutwe kama ilivyoamuliwa na Mahakama ya Haki ya Afrika Mashariki. (EACJ),” amesema Wakili Marenga.

Kwenye semina hiyo Deodatus Balile, Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) amesema, wameungana kwa pamoja katika kuhakikisha wanaweka mazingira rafiki kwa wanahabari kufanya kazi zao.

“Kuna sheria nyingi zilizowekwa na kulenga waandishi ama kushambulia tasnia, kwa tumeungana kwa pamoja kuhakikisha sheria hizo zinaondolewa makali yanayoumiuza wanahabari.

“Ni bahati nzuri sasa serikali nayo imeliona hili, mwelekeo wetu ua matumaini lakini tunapaswa kuendelea pamoja mpaka tunafikia lengo,” amesema Balile.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga kuongoza usambazaji wa mitungi ya gesi 10,000 ya Taifa Gas

Spread the loveNaibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga ameahidi kuongoza kwa ufanisi...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyabiashara, wawekezaji China waridhia kuwekeza bil. 800 katika sekta 5 nchini

Spread the loveUJUMBE wa wafanyabiashara na wawekezaji wakubwa kutoka Jimbo la Changzhou...

Habari Mchanganyiko

Bil. 4.42 kumaliza uhaba maji kata 2 Musoma Vijijini

Spread the loveWANANCHI wa kata za Busambara na Kiriba, Jimbo la Musoma...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Soko nepi za watoto lashuka, watu wazima lapaa

Spread the loveKiwanda cha kutengeneza nepi cha Japan kimetangaza kuwa kitaacha kutengeneza...

error: Content is protected !!