Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Magufuli amtisha Majaliwa
Habari za Siasa

Magufuli amtisha Majaliwa

Spread the love

JOHN Pombe Magufuli, Rais wa Tanzania amemtahadharisha, Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Kassim Majaliwa kuwa endapo atashindwa kutekeleza wajibu wake ipasavyo atamwondoa. Anaripoti Regina Mkonde…(endelea).

Rais Magufuli amesema hayo leo Jumatatu tarehe 16 Novemba 2020 mara baada ya kumaliza kumwapisha Majaliwa kuendelea kuwa waziri mkuu, hafla iliyofanyika Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma.

Pia, amewaapisha, Dk. Phillip Mpango kuwa Waziri wa Fedha na Mipango na Profesa Palamagamba Kabudi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Majaliwa ameapishwa kuendelea na wadhifa huo, baada ya ule wa miaka mitano ya utawala wa Rais Magufuli kumalizika tarehe 5 Novemba 2020 ambapo Rais Magufuli amemteua tena kuendelea kuhudumu nafasi hiyo.

Amesema, Tanzania mpaka sasa imeongozwa na mawaziri wakuu kumi kwa miaka tofauti tofauti akiwemo Majaliwa lakini anayeshikilia rekodi ya kuongoza kwa miaka kumi mfululizo ni; Frederick Sumaye.

Sumaye alikuwa waziri mkuu kati ya mwaka 1995-2005 enzi za utawala wa awamu ya tatu ya Hayati, Benjamin William Mkapa.

 

“Ukiangalia nafasi za uwaziri mkuu maana yake ni nafasi ambazo hazina uhakika, niliangalia vyombo vya habari na wengine wakishangilia kwamba Majaliwa amepata miaka mitano mingine kana kwamba niliwaambia atakaa miaka mitano,” amesema.

Rais Magufuli amesema, aliwaona baadhi ya wakazi wa Lindi wanafurahia na wengine wanajipongeza kwamba tumepata waziri mkuu kwa miaka mitano mingine.

“Nataka nimwambie kazi ya uwaziri mkuu haina uhakika, nilitaka nizungumze hili waziri mkuu aelewe, itategemea na utendaji kazi wake, kwa hiyo tumuombe ili angalau afikie kwenye rekodi ya Sumaye” amesema Rais Magufuli huku wageni waliokuwepo wakishangilia

Amesema, uhakika aliona ni miaka mitano iliyopita lakini hii mingine itategemea “lazima niwaeleze ukweli, kwa sababu sisi wanasiasa tunatabia ya kufurahi kufurahi, mimi nampa pole.”

“Na mama Majaliwa (Mary) jitahadhalishe kwenye hilo, anasema anakupa raha, huu ndio ukweli na hata kwa mawaziri hawa mawili na wengine nitakaowateua hawana uhakika,” amesema Rais Magufuli

Amesema, “sisi tumezunguka kwa wananchi kuwaomba kura, wametupa kura nyingi, lazima tulipe na kutimiza imani yao na hii ni kwa wote waliochaguliwa, makamu wa Rais, mimi na waziri mkuu na wabunge wote.”

Rais Magufuli amesema “katika miaka mitano iliyopita, waziri mkuu amefanya mambo ‘super’.Majaliwa anajituma nani mnyenyekevu.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

error: Content is protected !!