Friday , 26 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Magazeti yaliyofungiwa Tanzania kufunguliwa mwezi huu
Habari Mchanganyiko

Magazeti yaliyofungiwa Tanzania kufunguliwa mwezi huu

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Amon Mpanju
Spread the love

 

SERIKALI ya Tanzania, imesema mwezi huu wa Desemba 2021, huenda ukawa wa neema, kwa vyombo vya habari vilivyofungiwa. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Kauli hiyo ilitolewa jana Jumanne, tarehe 7 Desemba 2021, jijini Dar es Salaam na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Amon Mpanju, katika kikao kazi cha kuchambua mapendekezo 252, yaliyotolewa na Baraza la Haki la Umoja wa Mataifa (UN), kupitia kikao cha tatu cha tathimini ya mapitio ya hali ya haki za binadamu (UPR), kilichofanyika nchini Uswisi.

Ni baada ya washiriki wa kikao hicho kuilalamikia Serikali kushindwa kutekeleza mapendekezo ya baraza hilo la kuimarisha uhuru wa habari na wa kujieleza, ikiwemo kufungulia vyombo vya habari vilivyofungiwa kwa makosa mbalimbali.

Mpanju alisema, wizara husika imeshachukua hatua ya kulifanyia kazi suala hilo, kama ilivyoelekezwa na Rais Samia Suluhu Hassan, aliyeagiza vyombo vya habari vilivyofungiwa vifunguliwe.

“Kuhusu uhuru wa habari na vyombo vilivyofungiwa, wizara imechukua hatua na Rais Samia ameelekeza kwamba, lazima tulimalize. Najua na nina imani mwezi huu ukawa na neema, tutayamaliza,” alisema Mpanju.

Magazeti ambayo yalifungiwa na kumaliza adhabu zao na ma kusitishiwa leseni za uchapishaji na usambazaji; ni MwanaHALISI, Tanzania Daima, Mawio na Mseto.

Rais Samia aliagiza wizara husika, kuvifunguliwa vyombo vya habari vilivyofungiwa ili vianze kufanya kazi hukua akitaka sheria na taratibu kuzingatiwa.

1 Comment

  • Alisikika AKISEMA:-

    NIPE KIWANJA – (HALIMASHAURI YA TEMEKE IKAMPA BURE)

    NIJENGEE KWANGU – (NHC IKAFANYA KAZI)

    NYUMBANI KWANGU LETA MAJI – (MAMLAKA YA MAJI IKAFANYA KAZI)

    NYUMBANI KWANGU LETA UMEME – (TANESCO IKAFANYA KAZI)

    NYUMBANI KWANGU LETA SYSTEM YA MAJI MACHAFU – (MAMLAKA YA MAJI IKAFANYA KAZI)

    NYUMBANI KWANGU LETA BARABARA – (TANROAD IKAFANYA KAZI)

    NYUMBANI KWANGU LETA GOBOLE – (WIZARA YA ULINZI IKAFANYA KAZI)

    NYUMBANI KWANGU LETA MWANAMKE – (KAMPUNI YA WANAMWAKE IKAFANYA KAZI)

    KWELI ALIKUWA MWANAJESHI

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!