January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kauli ya Polepole yamponza, CCM yamjadili

Humphrey Polepole, Aliyekuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM

Spread the love

 

KATIBU Mkuu wa chama tawala nchini Tanzania- Chama Cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo amesema, kauli iliyotolewa na mbunge wake, Humphrey Polepole inajadiliwa na vikao husika. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Chongolo amesema hayo leo Jumatano, tarehe 8 Desemba 2021, alipokuwa akijibu swali la waandishi wa habari, mara baada ya kumaliza kutoa tathimini ya miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania Bara, ofisi ndogo za CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam.

Tanzania Bara kesho Alhamisi, inafikisha miaka 60 ya Uhuru uliopatikana 9 Desemba 1961 kutoka kwa Wakoloni. Sherehe hizo kitaifa zitafanyikia, Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam na mgeni rasmi atakuwa, Rais Samia Suluhu Hassan.

Chongolo mara baada ya kuelezea mafanikio yaliyopigwa, waandishi walimuuliza kauli aliyoitoa Polepole ambaye ni mbunge wa kuteuliwa aliyoitoa hivi karibuni kwamba, utawala wa awamu ya tano, haukuwamaliza wahuni wote.

“Je, mnawatambua hao wahuni na mkakati wa kuwaondoa ni nini,” ameluzwa Chongolo swali hilo na mmoja wa waandishi

Mtendaji mkuu huyo wa CCM akijibu swali hilo amesema ,“mimi siyo kikao, yanajadiliwa na vikao.” Hakuendelea kuelezea zaidi yah apo.

Kauli ya Polepole aliitoa wakati akihojiwa na Wasafi TV alipoulizwa kama kuna udhaifu katika utawala uliopita wa awamu ya tano uliokuwa ukiongozwa na Hayati Rais John Pombe Magufuli na mkamu wake, Samia Suluhu Hassan.

Polepole aliyewahi kuwa katibu wa itikadi na uenezi wa CCM kuanzia mwaka 2016 akichua kijiti kutoka kwa Nape Nnauye ambaye wakati huo aliteuliwa kuwa waziri wa habari, utamaduni, sanaa na michezo akisema, yeye (Polepole) alitamani “sana tuwe tumeshughulika na wahuni wengi tumewamaliza.”

“Lakini nafikiri Rais Magufuli na Mama Samia hawakufanikiwa kushughulika na wahuni, kwa hiyo tumebaki nao, kwa hiyo ukiniuliza jambo gani la udhaifu, nitakwambia bwana hatukufanikiwa kumaliza wahuni,” alisema Polepole, aliyewahi kuwa mjumbe wa iliyokuwa tume ya mabadiliko ya katiba.

Kauli hiyo, iliibua mjadala mkali mitandaoni huku Nape Nnauye ambaye ni Mbunge wa Mtama (CCM) mkoani Lindi kutumia ukurasa wake wa kijamii wa Twitter kuhoji “Du! Kumbe kulikuwa na orodha, natamani kujua wahuni waliopona.”

error: Content is protected !!