Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Madiwani Chadema, CUF Dar watimkia NCCR- Mageuzi
Habari za Siasa

Madiwani Chadema, CUF Dar watimkia NCCR- Mageuzi

Mustafa Muro, diwani wa Kinondoni (Chadema)
Spread the love

VIGOGO wawili wa upinzani jijini Dar es Salaam, Mustafa Muro (Chadema) na Maalim Amir Mbuju (CUF), wamekimbia vyama vyao na kujiunga na NCCR- Mageuzi. Anaripoti Hamis Mguta, Dar es Salaam … (endelea).

Madiwani hao; Mbunju wa Tandale na Muro wa Kinondoni wote katika Manispaa ya Kinondoni, wametangaza uamuzi huo leo Alhamisi tarehe 28 Mei, 2020 mbele ya waandishi wa habari, jijini Dar es Salaam.

Wawili hao wamesema, watajiunga rasmi NCCR- Mageuzi mara baada ya baraza la madiwani la manispaa ya Kinondoni kuvunjwa.

Akizungumza na waandishi wa habari Muro amesema, “Chadema kimesheheni uongozi usiokuwa na adabu na uliopoteza mwelekeo kutokana na chama chake kuwa na ubovu katika sehemu mblimbali.”

Amesema, ameamua kuondoka Chadema kwa hiari yake na kwamba anakwenda NCCR- Mageuzi, kwa sababu anaona ndiko upepo wa kisiasa unakoelekea.

Aidha, ameeleza ubovu huo ni pamoja na udhaifu wa kiuongozi, kuwa na viongozi waoga, kuwa waongo, kuwa na viongozi wasiojitambua pamoja na ukosefu wa adabu.

“Mara baada ya uchaguzi wa 2015 na yaliyotokea, (Freeman) Mbowe (mwenyekiti wa Chadema) na viongozi wengine walilewa sifa na kuanza kuona washauri sio kitu ila wapanda majukwaani ndio watu bora bila kukumbuka kuwa kinachoongewa majukwaani ni kile kilichochakatwa.”

“Hapa ndio nasema Mbowe ni kichwa cha nyoka na yeye kama kiongozi alitakiwa kuwa na maono kuhakikisha chama kinakuwa na wataalamu wa mikakati na wasemaji,” amesema.

Muro ambaye alijiunga na Chadema akitokea CCM tarehe 13 Octoba 2014 amesema, kitendo cha kuunda timu maalum ya Chadema ni msingi kwa kisingizio cha ujenzi wa chama kinadhihirisha uoga.

Amir Mbunju, diwani wa Tandale (CUF)

Kwa upande wake, Amir Mbunju amesema, anahamia NCCR Mageuzi kwa kuwa siasa ni upepo na katika uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 haoni kama chama cha CUF kinaweza kuhimili vishindo vya siasa kutokana na mgogoro uliokuwa ukiendelea ndani ya chama miezi kadhaa iliyopita.

Amesema kuhama kwake si kwa kutaka uongozi bali anaamini NCCR Mageuzi ndio sehemu sahihi kwenye upepo wa kisiasa.

Mbuju amewahi kuwa Naibu Meya wa Manispaa ya Kinondoni na Muro amepata kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Mipango Miji na mwenyekiti wa Madiwani wa Kanda ya Pwani.

Uamuzi huo wa madiwani, ni mwendelezo wa wanachama hasa wa Chadema kutangaza kutimkia NCCR- Mageuzi.

Tayari, wabunge wanne wa Chadema wamekwisha kutangaza mara baada ya Bunge hili la 11 kumaliza majukumu yake, watajiunga na NCCR- Mageuzi.

Wabunge hao ni: Joseph Selasini (Rombo), Anthony Komu (Moshi Vijijini), Susan Maselle na Joyce Sokombi wote wa viti maalum.

 

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

error: Content is protected !!