Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mabadiliko viongozi wa Serikali: Rais Samia afyeka, ateua wapya, wengine wahamishwa
Habari za SiasaTangulizi

Mabadiliko viongozi wa Serikali: Rais Samia afyeka, ateua wapya, wengine wahamishwa

Rais Samia Suluhu Hassan
Spread the love

RAIS Samia Suluhu Hassan ametengua uteuzi wa Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Omary Mgumba katika mabadiliko ya viongozi mbalimbali aliyoyafanya leo tarehe 26 Februari 2023. Anaripoti Jonas Mushi, Dar es Salaam … endelea)

Nafasi ya Ndaki imechukuliwa na aliyekuwa Naibu wake, Abadallah Ulega huku nafasi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga ikichukuliwa na Waziri Kindamba ambaye amehamishwa kutoka mkoa wa Songwe. Rais Samia amemteua Dk. Francis Michael kuwa Mkuu wa Mkoa wa Songwe.

Pia katika mabadiliko hayo yaliyogusa Mawaziri, Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu, Naibu Makatibu Wakuu, Wakuu wa Mikoa na Mkurugenzi wa Uchaguzi, wapo wapya waliochomoza huku wengine wakihamishwa vituo vyao vya kazi.

Jina la Mbunge wa Muheza, Hamis Mwinjuma maarufu Mwana FA ni miongoni mwa majina mapya yaliyochomoza ambapo ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo akichukua nafasi ya Paul Gekul aliyehamishiwa Wizara ya Katiba na Sheria.

Taarifa ya mabadiliko hayo imetolewa leo Jumapili tarehe 26 Februari 2023 na Katibu Mkuu Kiongozi, Dk. Moses Kusiluka, ambapo amesema Rais Samia amemwamisha Naibu Waziri wa Radhi Nyumba na Maendeleo ya Makzi, Ridhiwani Kikwete kwenda kuwa Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

Kwa upande wa makatibu wakuu wapya Rais Samia amemteua Tausi Kida (Ofisi ya Rais Uwekezaji); Juma Mkomi (Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora); Balozi Samwel Shelukindo (Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki); Prof. Carolyne Nombo (Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia).
Makatibu Wakuu wengine ni Gerald Mweli (Wizara ya Kilimo); Dk. Seif Shekalaghe (Wizara ya Afya); Mhandisi Nadhifa Kemikimba (Wizara ya Maji); Kheri Mahimbali (Wizara ya Madini)Mohamed Hamis (Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari).

Makatibu Wakuu waliobadilishwa Wizara ni pamoja na Rizki Shemdoe kutoka Kutoka Ofisi ya Rais Tawala za mIkoa na Serikali za Mitaa kwenda Wizara ya Mifugona Uvuvi; Dk. John Jingu kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge kwenda Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum na Dk. Jim Yonazi kutoka Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Hanbari kwenda Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge.

Wengine ni Adolf Ndunguru kutoka Wizara ya Madini kwenda Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na seriaklli za Mitaa (Afya) na Mhandisi Anthony Sanga kutoka Wizara ya Maji kwenda Wizar ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

Aidha Rais amewateua Naibu Makatibu Wakuu wapya wakiwemo Dk. Wilson Mahera (Ofisi ya Rais Taawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI); Sospeter Mwale (Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi)); Dk. Franklin Rwezimula (Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia (Elimu ya Msingi na Sekondari)).

Manaibu Katibu Wakuu wapya wengine ni Hussein Omar, (Wizara ya Kilimo); Cyprian Luhemeja, (Wizara ya Maji); Lucy Kabyemera (Wizara ya Maliasili na Utalii); Anderson Mutatembwa, (Wizara ya Maaliasili an Utalii) na Athuman Mbuttuka (Wizara ya Nishati); Dk. Daniel Mushi(Wizara ya Mifugo na Uvuvi (mifugo)), Agnes Meena(Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi)) na Selestine Kakele (Wiara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari).

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

error: Content is protected !!