March 2, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Maalim Seif mguu nje, mguu ndani CUF

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad akifunga mkutano wa kujadili amani na utulivu nchini

Spread the love

TAMKO la Maalim Seif Shariff Hamad, Katibu Mkuu wa CUF kwamba ‘muda ukifika nitazungumza’ kuhusu kuhama chama hicho inatikisa msimamo wake wa awali. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Tamko hilo amelitoa ikiwa ni siku nne baada ya kupata ‘mwaliko’ wa kujiunga na Chadema ambapo ameahidiwa kugombea nafasi ya urais visiwani Zanzibar kwenye Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020.

Ahadi hiyo ya Chadema ilitolewa na Hashim Juma, Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa Chadema.

Maalim Seif amesema kwamba, kwa sasa hawezi kuzungumzia suala la kwenda Chadema kwa sasa na kwamba, wakati ukifika atazungumza na waandishi.

Kauli ya Maalim Seif iliwasilishwa na Nassor Ahmad Mazrui, Naibu Katibu Mkuu wa CUF-Zanzibar

Kauli hiyo ya Maalim Seif inaonesha kulegeza msimamo wake wa awali kwamba hawezi kuhama CUF.

Msimamo huo unafanana na ule wa Ally Saleh, Mbunge wa Malindi (CUF) kwamba, wakati ukigika watajua wafanye nini ili wabaki kwenye Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).

Tayari Magdalena Sakaya, Naibu Katibu Mkuu CUF Bara amemtahadharisha Maalim Seif kwamba, akihama CUF itakuwa ndio mwisho wake wa siasa.

error: Content is protected !!