October 2, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Maalim Seif atikiswa Pemba

Maalim Seif Shariff Hamad

Spread the love

AHMED Ngwali, Mbunge wa Wawi mkoani Kusini Pemba kupitia Chama cha Wananchi (CUF), amejivua uanachama na kuhamia Chama Cha Mapinduzi (CCM). Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Pembe iliyokuwa ngome ya CUF, kwa sasa ni ngome ya Chama cha ACT-Wazalendo ambapo Maalim Seif Sharif Hamad ndio mshauri mkuu wa chama hicho.

Ngwali ametangaza uamuzi huo leo tarehe 2 Machi 2020, katika ziara ya Humphrey Polepole, Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM, ya kukagua miradi ya maendeleo visiwani Pemba.

Mwanasiasa huyo amesema, ameamua kujivua uanachama wa CUF pamoja na kujiuzulu ubunge, baada ya kuridhishwa na kasi ya utendaji kazi wa serikali iliyoko madarakani.

“Kwa niaba ya wananchi wa Ziwani leo tarehe 2 Machi 2020, kwa matendo ya CCM mnayofanya naamua kujivua ubunge na kujivua vyeo vyangu vyote vya chama, kuacha kiinua mgongo, kuacha posho za vikao, kwa ajili ya wananchi wetu hawa,” amesema Ngwali.

Ngwali anakuwa mbunge wa kwanza wa upinzani visiwani Zanzibar kuhamia CCM, baada ya sakata hili kushika kasi Tanzania Bara.

Taarifa zaidi zinaeleza, wabunge wengi Pemba wamekuwa watiifu kwa uongozi wa ACT-Wazalendo, huku alama na bendera za CUF zikielekea kutoweka kisiwani humo.

Hata hivyo imeelezwa, wabunge kwenye kisiwa hicho wamekuwa wakishawishiwa kujiunga CCM, kwa ahadi ya ‘kupatiwa’ ubunge kwenye uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu.

error: Content is protected !!