September 23, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Maafisa wa Serikali wafundwa ulinzi wa haki za binadamu

Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Tanzania (THBUB), Mohamed Hamis Hamad

Spread the love

 

MAAFISA wa Taasisi za Serikali zinazoshughulika na masuala ya haki za binadamu, wametakiwa kushrikiana na Asasi za Kiraia na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGO’s), katika kuimarisha ulinzi wa haki hizo nchini. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Wito huo umetolewa leo Jumanne, tarehe 3 Julai 2021 na Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Tanzania (THBUB), Mohamed Hamis Hamad, katika semina ya kuwajengea uwezo maafisa wa Serikali na watetezi wa haki za binadamu, iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

“Suala la haki za binadamu inahitaji ushirikiano wa wote, maafisa wa Serikali watatumia nafasi yao kuingiza masuala hayo katika mipango ya Serikali. Kama ni kwenye sheria, mikakati, sera au katika masuala mbalimbali ya utetezi wa haki za binadamu,” amesema Hamad.

Hamad amesema, maafisa wa Serikali wana nafasi kubwa katika kuhakikisha wanaotetea haki za binadamu, haki zao zinalindwa kisheria.

“Kama masuala ya kisheria, anayetunga sheria ni Serikali. Serikali inaanzisha suala inapeleka bungeni muswada wa sheria. Kama ni masuala ya sera, anayetunga sera ni Serikali. Hawa wadau wana nafasi kubwa katika masuala ya haki za binadamu,” amesema Hamad.

Semina hiyo ya kuwajengea uwezo maafisa wa Serikali, katika taasisi zinazoshughulika na masuala ya haki za binadamu, imeandaliwa na Mtandao wa Uhamasishaji wa Kitaifa wa Haki za Binadamu Afrika, kwa kushirikiana na THBUB.

Pamoja na mambo mengine, semina hiyo imelenga kuwaejengea uwezo maafisa wa Serikali na watetezi wa haki za binadamu nchini, juu ya utekelezaji wa azimio la Marrakech lililopitishwa 2018 nchini Morocco, kwa ajili ya kulinda haki za binadamu ikiwemo za waumini wa dini ya Kiislamu.

Mratibu wa Mtandao wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), Onesmo Olengurumwa, amesema mafunzo hayo yatasaidia kuimarisha uhusiano kati ya maafisa wa Serikali na watetezi wa haki za binadamu, katika utekelezaji majukumu yao ya kulinda haki hizo.

“Mafunzo haya yanatufanya tuweze kuonesha namna gani tunapaswa kushirikiana, kati ya watetezi wa haki za binadamu na taasisi za Serikali ambazo zinahusika moja kwa moja na haki za binadamu. Ndiyo maana tumekutana hapa tunataka kuonyesha kwamba, kazi zetu zinaingiliana hata kama uko serikalini,” amesema Olengurumwa.

Olengurumwa amesema, maafisa hao wa taasisi za Serikali wakitekeleza majukumu yao vizuri, watasaidia kuimarisha misingi ya haki hizo nchini.

Mwanaharakati huo ametaja mifano ya taasisi hizo kuwa ni, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) na Jeshi la Polisi.

“Ukiwa mtetezi wa haki za binadamu kazi yako itakuwa nzuri, mfano ukiwa Takukuru ukiheshimu haki za binadamu utatetea wale wanaoathirika na rushwa, ukiwa Polisi ulikilinda haki za binadamu utatetea wale ambao haki zao zinavunjwa kinyume cha sheria, kila mtu akisimama kwa sheria haki zitalindwa,” amesema Olengurumwa.

error: Content is protected !!