Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Lukuvi afanya yake Monduli
Habari za Siasa

Lukuvi afanya yake Monduli

Spread the love

WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi ameagiza kufukuzwa kazi afisa ardhi wa wilaya ya Monduli Kitundu Mkumbo. Anaandika Mwandishi Wetu … (endelea).

Sababu ya agizo ni kwamba, Mkumbo amekiuka sheria na taratibu za utoaji wa hati miliki za kimila.

Lukuvi ametoa agizo hilo mbele ya wakazi wa Kijiji cha Engarooji wilayani Monduli mkoani Arusha ambao wamekua katika mgogoro wa ardhi kwa muda mrefu hivyo kugawika katika makundi mawili yasiyoelewana.

Lukuvi amefafanua kuwa, mwenye mamlaka ya kumilikisha mtu ardhi zaidi ya hekari 50 ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pekee.

“Afisa huyu wa ardhi ambaye japo hapo awali mlishawahi kumsimamisha kazi kwa makosa mengune kama haya, lakini kwa sasa makosa haya ni makubwa sana na sasa afukuzwe kazi, haiwezekani amilikishe hekari zaidi ya 1,500 kinyume na sheria” Alisema Lukuvi.

Katika hatua nyingine Lukuvi amezifuta hati zote za kimila zilizotolewa na afisa ardhi huyo kwasababu zimetolewa kinyume na utaratibu kwa mujibu wa sheria ya ardhi ya mwaka 1999 ambayo hairuhusu kutoa hatimiliki za kimila zaidi ya hekari 50 bila idhini ya Rais.

Miongoni mwa watu waliomilikishwa maeneo makubwa kubwa katika kijiji cha Engarooji wilayani Monduli ni Paulo Ndari mwenye hekari 716, Lekashu Ng’ene mwenye hekari 301 na Salimu Orkoskos mwenye hekari 268.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

error: Content is protected !!