May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Liverpool dhidi ya Manchester United kuamua ubingwa wa Man city

Spread the love

 

MCHEZO wa Ligi Kuu nchini England kati ya Liverpool dhidi ya Manchester United utamua hatma ya ubingwa wa Manchester City kwa msimu wa 2020/21. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Mchezo huo utapigwa hii leo kwenye Uwanja wa Anfield jijini Liverpool majira ya saa 12 jioni.

Katika mchezo huo kama Manchester United atafungwa klabu ya Manchester City itatangazwa kuwa mabingwa wapya wa Ligi Kuu nchini humo huku ikiwa imesalia michezo minne.

Manchester United kwa sasa inapointi 67 ikiwa imecheza michezo 33, kama ikipoteza kwenye mchezo wa leo dhidi ya Liverpool hatoweza kufikia alama za Manchester City ambao wapo kileleni wakiwa na pointi 80 hata wakishinda michezo yao minne ya mwisho.

Kama Manchester United watapata ushindi leo watakuwa wanafikisha pointi 70, ambapo itawalazimu Manchester City kushinda mchezo wao unaokuja ili kutangazwa kuwa mabingwa wapya wa taji hilo.

Liverpool inaingia kwenye mchezo huo huku ikiwa kwenye nafasi ya sita wakiwa na pointi 56 ambapo wanahitaji ushindi ili waweze kujisogeza katika nafasi nne za juu ili kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa msimu ujao.

error: Content is protected !!