Friday , 2 June 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Lissu: Safari hii tutafanya kama CCM
Habari za Siasa

Lissu: Safari hii tutafanya kama CCM

Tundu Lissu, Mgombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chadema
Spread the love

TUNDU Lissu, mgombea urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), amesema wataweka kituo cha kuhesabu kura zao kama Chama Cha Mapinduzi (CCM). Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Amesema, watatengeneza mfumo wa kuhakikisha kura zao haziibwi, na pia watahakikisha wanakuwa na vituo vyao kwa ajili ya kukusanya data za matokeo kutoka kila kituo cha uchaguzi nchi nzima.

Lissu ambaye anagombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mara ya kwanza, amesema chama chake kinatengeneza mazingira ya kuhakikisha kama kitashindwa, basi kinashindwa kihalali kwenye uchaguzi unaotarajiwa kufanyika tarehe 28 Oktoba 2020.

Amesema, mwaka 2015 walikuwa na eneo walilolitenga kwa ajili ya kukusanya data za matokeo yao ya urais kutoka kila eneo, hata hivyo walivamiwa na polisi.

“Tulikusanya matokeo yetu mwaka 2015, tukavamiwa na polisi. Kisheria sio kosa kukusanya matokeo yako mwenyewe. Tutakuwa na utaratibu utakaohakikisha kwamba matokeo ya urais tunayajumlisha wenyewe. Tutafanya kama mwaka 2015, tutakusanya kutoka kwenye vyanzo vyetu kwa mawakala. CCM wana vituo vyao na sisi tutakuwa na vituo vyetu vya kukusanya data.

“Mwaka huu kutakuwa na ugomvi wa kutengeneza. Mnafahamu mambo yaliyotokea kwenye chaguzi za marudio jinsi ilivyokuwa ngoma nzito kama uchaguzi wa Kinondoni. Uchaguzi wa safari hii ngoma itakuwa kubwa kweli kweli,” amesema wakati akizungumza na wahariri na wanahabari nyumbani kwake jijini Dar es Salaam.

Amesema, ugumu mwingine kwenye uchaguzi huo unahusu kanuni inayoeleza kuwa, fomu za matokeo zitagawiwa kwa mawakali kama zitakuwepo.

“Tunaisihi tume (Tume ya Taifa ya Uchaguzi) kutoa fomu kwa idadi ya wagombea wa urais na wabunge, msipofanya hivyo itakuwa ni namna ya kwanza ya kuiba kura,” amesema Lissu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Lusinde: CCM hatuliachii ng’o jimbo la Moshi Mjini

Spread the loveMJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (NEC), Livingston...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar: Bakharesa hajavamia shamba letu

Spread the love  IKULU Visiwani Zanzibar, imeeleza kuwa eneo la kiwanda cha...

Habari za SiasaTangulizi

Zanzibar watangaza rasmi kuwa shamba la Razaba ni mali yao

Spread the love  SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), imetangaza rasmi kwamba shamba...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Mwinyi azindua Kamati ya Maridhiano Visiwani

Spread the love  RAIS wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Dk. Hussein...

error: Content is protected !!