TUNDU Lissu, Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) amesema, anarejea nyumbani kwao Tanzania lakini alivyo sasa si kama alivyokuwa miaka mitatu iliyopita. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Lissu aliondoka nchini usiku wa tarehe 7 Septemba 2017 akiwa hajitambuia kupelekwa Hospitali Nairobi nchini Kenya akitokea Hospitali ya Rufaa Dodoma, Tanzania alipokuwa amepelekwa mchana wa siku hiyo baada ya kushambuliwa na watu wasiojulikana.
Mwanasiasa huyo alishambuliwa kwa risasi zaidi ya 30 kati yake 16 zilimpata mwilini. Tangu wakati huo amekuwa akipata matibabu Nairobi kasha tarehe 6 Januari 2018 alihamishiwa nchini Ubelgiji kwa matibabu.

Tayari amekwisha kupona na kesho Jumatatu tarehe 27 Julai 2020 saa 7:20 mchana anarejea kwa ndege ya Shirika la Ndege la Emirates akitoa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam.
Akizungumza na mtandao wa chombo cha habari cha Daily Nation leo Jiumapili tarehe 26 Julai 2020, akiwa kwenye maandalizi ya kurejea Tanzania, Lissu amesema, viungo vyake vina afya njema lakini havipo kama vilivyokuwa kabla ya kushambuliwa.
“Miguu yangu yote, kiuno changu, mikono yangu na tumbo langu vimeshambuliwa. Hivyo, kurudi katika hali ya kawaita itachukua muda mrefu,” amesema Lissu.

“Afya yangu ni nzuri kabisa ingawa sipo kama nilivyokuwa miaka mitatu iliyopita, lakini niseme nipo sawasawa. Ninajivuta vuta kidogo lakini ukiachana majeraha ya kushambuliwa, nipo vizuri.”
Kuhusu siasa za Tanzania na uchaguzi mkuu wa tarehe 28 Oktoba 2020 ambapo yeye ni miongoni mwa watia nia ya kugombea urais wa Tanzania ndani ya Chadema, amesema, tatizo kuba lipo kwenye uchaguzi huru na kuonesha mashaka baada ya upigaji kura kwenye uchaguzi huo.
Amesema, yapo matukio ambayo yamewafanya Watanzania kuwa waoga na kwamba, hilo ndio tatizo kubwa linaloikabili Tanzania kwa sasa.
Leave a comment