PAZIA la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) 2019/20 limefungwa leo huku timu za Singida United, Ndanda ya Mtwara, Lipuli ya Iringa na Allience ya Mwanza zikishuka daraja. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Mbali za timu hizo nne kushuka daraja msimu huu, lakini Mbeya City na Mbao FC wanatakiwa kucheza hatua ya mtoani na timu za ligi daraja la kwanza ili kugombania kubaki katika ligi hiyo msimu ujao.
Ligi hiyo iliyomalizika kwa Simba kutwaa ubingwa ikiwa na pointi 88 huku nafasi ya pili ikishindwa na Yanga ikiwa na pointi 72 na Azam FC wakiwa nafasi ya tatu wakiwa nafasi ya 70.
Singida United iliyoshuka daraja mapema kabla ya ligi hiyo kumalizika, leo wamekubali kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Biashara United, hivyo wamejihakikishia kushuka daraja.

Mbao FC ilizima ndoto za Ndanda FC kubaki katika Ligi Kuu Bara baada ya kuichapa mabao 2-0, hivyo kuaga ligi hiyo ikiwa nafasi ya 19 ikivuna pointi 41 baada ya kucheza mechi 38.
Lipuli wameipa kisogo ligi hiyo baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0 dhidi ya Yanga, hivyo kumaliza ikiwa na pointi 44.
Alliance FC pamoja na kushinda mabao 3-2 dhidi ya Namungo FC na kufikisha pointi 45 lakini pointi hazikutosha kubaki katika msimu huo, wamelazimika kushuka daraja wakiwa katika nafasi ya 17 katika msimamo wa ligi hiyo.
Mbeya City na Mbao ambao zina kibarua cha kupigania kubaki Ligi Kuu msimu ujao wamemaliza ligi kuwa na pointi 45 kila mmoja wakizidiana mabao ya kufunga na kufungwa.
Leave a comment