Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Lissu kupokelewa kwa maandamano
Habari za Siasa

Lissu kupokelewa kwa maandamano

Spread the love

WANACHAMA na wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), watamsindikiza Tundu Lissu kwa maandamano kutokea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere hadi Makao Makuu ya chama hicho, Kinondoni, Dar es Salaam. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Taarifa hiyo imetolewa leo Jumatatu tarehe 27 Julai 2020 na Hemed Ally, Katibu wa Chadema Kanda ya Pwani, akizungumza na wanahabari uwanjani hapo.

Lissu alikuwa nje ya nchi kwa takribani miaka mitatu kwa ajili ya matibabu, baada ya kushambuliwa na risasi na watu wasiojulikana, tarehe 7 Septemba 2020, jijini Dodoma.

Hemed amesema, wafuasi wa Chadema wameamua kumsindikiza Lissu kwa maandamano hadi makao makuu ya chama hicho, ikiwa ni sehemu ya kuonyesha furaha yao juu ya ujio wa kiongozi huyo.

“Ni haki yetu kumpokea Lissu na tutamsindikiza kwa maandamano hadi makao makuu ya chama. Polisi wanatekeleza wajibu wao lakini na sisi ni haki yetu kumpokea kiongozi wetu aliyekuwa nje ya nchi kwa muda mrefu,” amesema Hemed.

Awali, kundi la wafuasi wa Chadema walizuiliwa kuingia uwanjani hapo, lakini baadae polisi waliwaruhusu waingie ndani.

Tayari Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema na John Mnyika, Katibu Mkuu wa chama hicho wapo uwanjani hapo.

Wapenzi wa Chama cha Chadema wakiwa nje ya uwanja wa Ndege wa JK Nyerere

Endelea kufuatilia MwanaHALISI Online, MwanaHALISI TV na mitandao yetu ya kijamii kwa habari zaidi

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

error: Content is protected !!