Saturday , 3 June 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Wamiminika kumpokea Lissu
Habari za Siasa

Wamiminika kumpokea Lissu

Wapenzi wa Chama cha Chadema wakiwa nje ya uwanja wa Ndege wa JK Nyerere
Spread the love

BAADHI ya wanachama na viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), wamejitokeza Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kumpokea Tundu Lissu. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Lissu anarejea leo Jumatatu tarehe 27 Julai 2020 akitoka nchini Ubelgiji alikokuwa akipata matibabu baada ya kushambuliwa kwa risasi zaidi ya 30 na watu wasiojulikana mchana wa tarehe 7 Septemba 2017 mjini Dodoma.

Kadri muda unavyokwenda, viongozi na wanachama wa Chadema wanamiminika uwanjani hapo ili kumpokea Lissu, Makamu Mwenyekiti wa chama hicho anayetarajia kutua saa 7:20 mchana kwa ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia.

          Soma zaidi:- 

Miongoni waliofika kumpokea ni, Alute Mughwai, kaka yake na Vicent ambaye ni mdogo wake.

Pia, waliokuwa wabunge wa chama hicho, John Heche (Tarime Vijijini), Joseph Mbilinyi maarufu Sugu (Mbeya Mjini), Godbless Lema (Arusha Mjini), mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Iringa, William Mungai na aliyekuwa Meya wa Ubungo, Boniface Jacob.

MwanaHalisi Online lililopo uwanjani hapo, limeshuhudia utulivu ukiendelea.

Endelea kufuatilia MwanaHALISI Online, MwanaHALISI TV na mitandao yetu ya kijamii kwa habari zaidi

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Lusinde: CCM hatuliachii ng’o jimbo la Moshi Mjini

Spread the loveMJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (NEC), Livingston...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar: Bakharesa hajavamia shamba letu

Spread the love  IKULU Visiwani Zanzibar, imeeleza kuwa eneo la kiwanda cha...

Habari za SiasaTangulizi

Zanzibar watangaza rasmi kuwa shamba la Razaba ni mali yao

Spread the love  SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), imetangaza rasmi kwamba shamba...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Mwinyi azindua Kamati ya Maridhiano Visiwani

Spread the love  RAIS wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Dk. Hussein...

error: Content is protected !!