October 1, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Lissu ampa kibano IGP Sirro

Tundu Lissu, aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki

Spread the love

HATUA ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro kudai uchunguzi wa shambulio la Tundu Lissu unakwama kutokana na kutokuwepo kwake nchini, imejibiwa vikali. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Lissu ambaye ni Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), amesema sheria za nchi zinampa haki ya kuendelea na uchunguzi.

Jana tarehe 18 Novemba 2019, IGP Sirro alisema, Jeshi la Polisi linamsubiri Lissu, ambaye ni mhanga wa shambulio, arejee ili waanze upelelezi.

Kutokana na kauli hiyo, Lissu amesema yeye na dereva wake hawalizuii kuchunguzwa shambulio la risasi dhidi yake.

“Unadai Jeshi la Polisi linashindwa kuchunguza shambulio dhidi yangu, kwa sababu mimi na dereva wangu tuko nje ya nchi? Je, mimi na dereva wangu tumekuzuia kuwasiliana na Interpol ili waje kuchukua ushahidi wetu kama mapolisi wako wanashindwa kuja tuliko Ulaya kutuhoji?” amehoji Lissu.

Amesema, sheria za nchi zimeipa Jamhuri mamlaka ya kuchunguza, kufungua na kuendesha kesi za jinai.

“Unadai mnanisubiri mimi nije kufungua kesi ya kushambuliwa kwangu? Mimi sio Jamhuri, sheria zetu zimeipa Jamhuri mamlaka ya kuchunguza, kufungua na kuendesha kesi zote za jinai nchini kwetu.

“Wewe na Jeshi lako mnalipwa mshahara kwa kodi zetu ili mfanye kazi hiyo,” ameeleza Lissu.

Mara kadhaa Jeshi la Polisi limeeleza kuwa, upelelezi wa tukio hilo unakwamishwa na mhusika (Lissu), kushindwa kutoa ushirikiano.

error: Content is protected !!