Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Lissu aibua shangwe mkutano mkuu ACT-Wazalendo
Habari za Siasa

Lissu aibua shangwe mkutano mkuu ACT-Wazalendo

Spread the love

TUNDU Antipus Lissu, mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), ameibua shangwe ndani ya Mkutano Mkuu wa ACT-Wazalendo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Mkutano huo unafanyika leo Jumatano tarehe 5 Agosti 2020 katika ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam.

Lissu ameingia ukumbini wakati Zitto Kabwe, Kiongozi wa ACT-Wazalendo akijiandaa kutoa hotuba kwa wajumbe wa mkutano huo.

Kabla hajaanza, Lissu ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Chadema-Bara, akaingia ukumbini akiwa ameambatana na mgombea wake mwenza, Salum Mwalimu ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu-Zanzibar.

Shangwe ziliibuka kwa wajumbe kusimama kushangilia wakiimba wimbo maalum wa ACT-Wazalendo huku Lissu akisalimiana na wajumbe na viongozi mbalimbali.

Kabla hajakaa katika nafasi iliyokuwa imeandaliwa, Zitto alimwita Lissu na Bernard Membe, Mshauri Mkuu wa ACT-Wazalendo wapande jukwaani hali iliyoibua shangwe zaidi. Membe anatarajiwa kuteuliwa na mkutano huo kuwa mgombea urais

Watatu hao walikaa jukwaani kwa muda huko wakiimba wimbo na kuwasalimia wajumbe wa mkutano huo.

Katika hotuba yake, Zitto amesema, “nimefurahi kuwaona wagombea wetu wawili wa urais wakiwa pamoja na kwetu sisi kushirikiana ni muhimu na bila kushirikiana itakuwa ni ngumu kuindoa CCM madarakani na itakuwa rahisi mmo kuiondoa CCM madarakani.”

Ziito amesema, “tutaendelea kufanya mazungumzo hadi hatua ya mwisho kuhakikisha tunashirikiana na kuwa na mgombea mmoja.”

Endelea kufuatilia MwanaHALISI Online, MwanaHALISI TV na mitandao yetu ya kijamii kwa taarifa na habari mbalimbali.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

error: Content is protected !!