Ligi kuu ya soka Tanzania Bara msimu wa 2022/23 kuanza kutimua vumbi leo 15 Agosti 2022 kwa kushuhudia mechi mbili katika viwanja viwili tofauti ambapo Ihefu watakuwa wenyeji wa Ruvu Shooting huku Mtibwa Sugar akiwa mgeni wa Namungo katika ufunguzi huo wa Ligi . Anaripoti Damas Ndelema
Michezo wa kwanza utapigwa majira ya saa kumi kamili katika kiwanja cha Highland Estate uliopo mbeya ambao ni uwanja wa nyumbani wa klabu ya Ihefu ambayo imepanda daraja msimu huu ikitokea ligi daraja la kwanza ambapo katika mchezo huo watawakaribisha maafande wa Ruvu shooting ya pwani na kila mmoja kutafuta alama tatu muhimu
Huku mchezo mwingine ukichezwa majira ya saa moja jioni ambapo Namungo watawakaribisha mtibwa Sugar katika dimba la Benjamin Mkapa ambao ndio utakuwa uwanja wao wa nyumbani mpaka pale uwanja wao wa Majaliwa ambao upo kwenye marekebisho hivyo wataanza harakati za kusaka ubigwa wa NBC leo dhidi ya wakata miwa hao wa Manungu katika dimba hilo la Benjamin Mkapa
Mashabiki wengi wa soka nchini walikua wakisubiri kwa hamu kurejea kwa Ligi kuu Tanzania Bara kutokana na usajili uliofanywa na timu zote katika dirisha hili la usajili huku ikitegemewa ligi hii itakuwa na ushindani mkubwa kutoka na sajili mbalimbali zilizofanywa kwani kuna wachezaji mbalimbali kutoka Afrika mpaka nje ya Bara hili la Afrika
Leave a comment