
Maria Sarungi Tsehai, Mkurugenzi wa Kampuni ya Kwanza Broadcasting Limited
KAMPUNI ya Kwanza, inayoendesha Televisheni ya mtandaoni (Kwanza TV), inatarajia kukata rufaa dhidi ya hukumu ya kufungiwa chaneli yake, kwa muda miezi sita. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).
Taarifa hiyo imetolewa leo tarehe 24 Oktoba 2019 na Maria Sarungi, Mkurugenzi wa Kampuni ya Kwanza Broadcasting Limited.
Taarifa ya Sarungi imeeleza kuwa, amedhamiria kupinga hukumu hiyo namba 5 iliyotolewa mwezi Septemba 2019 na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) chini ya Kamati yake ya Maudhui.
Maria ameeleza kuwa, rufaa hiyo imekatwa katika Baraza la Rufaa la Tume ya Ushindani Tanzania.
More Stories
Barrick ilivyoshiriki katika kuadhimisha Siku ya Canada
PURA yaanzisha kanzidata
Branch kufikisha mikopo ya haraka kwa mamilioni ya Watanzania