Thursday , 25 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Bimani aeleza machungu siasa za upinzani
Habari za SiasaTangulizi

Bimani aeleza machungu siasa za upinzani

Kaimu Naibu Katibu Mkuu ACT-Wazalendo-Zanzibar, Salim Bimani (Picha na Mintanga Hunda)
Spread the love

SALIM Bimani, Mwenyekiti wa Kamati ya Itikadi, Uenezi, Mawasiliano na Umma wa Chama cha ACT Wazalendo,  amesema kitendo cha vyama vya siasa, kuzuiwa kufanya shughuli za siasa, ni sawa na kuzuia maji kuteremka kwenye mto. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Bimani ametoa kauli hiyo leo tarehe 24 Oktoba 2019,  jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na wanahabari.

“Tumeshuhudia matukio mbalimbali, ukosefu wa demokrasia, uvunjifu wa haki za binadamu na katiba unaofanywa na CCM. Ubakwaji wa demokrasia, ukiukwaji wa Katiba na Sheria ya Vyama vya Siasa,” amesema Bimani na kuongeza:

“Chama cha kisiasa kina haki ya kufanya mikutano ya hadhara, maandamano na makongamano sababu kinaeleza sera zake, mwaka wa nne huu chama cha CCM kimedhibiti vyama vingine visifanye shughuli za siasa, lakini ni bure kuzuia maji yasiteremke kwenye mto, maji yanateremka kwa kasi.”

Bimani ameeleza kuwa, hasira za vyama vya siasa kuzuiwa kufanya shughuli zake, zitaonekana katika uchaguzi ujao wa serikali za mitaa.

Amesema, vyama vya upinzani vitakipa kipigo cha mbwa koko, Chama Cha Mapinduzi (CCM).

“Sasa malipo ya kutuzuia, tuyaoneshe kwenye serikali za mitaa, wapate kipigo cha mbwa koko waone Watanzania hawaridhiki na hali hiyo, viongozi wote tunapaswa kushughulikia hilo,” amesema Bimani.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

error: Content is protected !!