July 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Upelelezi kesi ya Kabendera danadana

Mwandishi Erick Kabendera akiwa mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu

Spread the love

UPANDE wa Mashtaka wa kesi inayomkabili mwandishi wa habari za uchunguzi nchini, Erick Kabendera, umedai bado upepelezi haujakamilisha. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Leo tarehe 24, Oktoba 2019, Wakili Mwandamizi wa Serikali Wankyo Simon mbele Hakimu Mkazi, Victoria Mwaikambo ameieleza mahakama kuwa shauri hilo lipo kwa ajili ya kutajwa na kwamba upelelezi haujakamilika. 

Upande wa utetezi umewakilishwa na Wakili Leonard Martin. Shauri hilo limeahirishwa hadi tarehe 7 Novemba, 2019.

Awali tarehe 11 Oktoba, mwaka huu, Wakili wa anayemtetea Kabendera, Jebra Kambole aliiarifu mahakama kuwa Kabendera anaomba kuzungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Mashtaka (DPP), juu ya kuomba kusamehewa makosa yake.

Kabendera anashtakiwa Mahakamani hapo kwa makosa matatu ikiwemo kujihusisha na mtandao wa uhalifu, kukwepa kodi kiasi cha Sh.173.3 milioni na utakatishaji fedha haramu kiasi cha Sh.173.3 milioni.

error: Content is protected !!