Tuesday , 5 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Kusimamishwa uwakili; Fatma atuma ujumbe kwa JPM
Habari za SiasaTangulizi

Kusimamishwa uwakili; Fatma atuma ujumbe kwa JPM

Fatuma Karume, aliyekuwa Rais wa Chama cha Wanasheria Tanzania (TLS)
Spread the love

WAKILI Fatma Karume amemueleza Rais John Magufuli kwamba, yuko tayari kukaa jela miaka 30, ili kuboresha demokrasia na utawala wa sheria nchini. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Fatma ametoa kauli hiyo jana tarehe 20 Septemba 2019 kupitia ukurasa wake wa Twitter, saa kadhaa baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, kumsimamisha uwakili kwa muda ikimtuhumu kutoa kauli za kuishambulia Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

“Nimemalizika kwa kunifungia uwakili?Nyinyi mnaendeshwa kwa njaa ya matumbo yenu na si njaa ya haki! Mwambieni Rais Magufuli niko tayari kufa kwa Demokrasia na Utawala wa Sheria. Wasiojulikana wanajua nakaa wapi waje tu,” amesema Fatma.

Fatma aliyewahi kuwa Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) amesema kitendo cha kusimamishwa uwakili, hakitoshi kulipia thamani ya demokrasia na utawala wa sheria.

“Rais Magufuli nataka uelewe niko tayari kukaa jela miaka 30 kama kukaa kwangu jela italeta demokrasia na utawala wa sheria nchi hii.Kwa hivyo kuchukua haki yangu ya kusimamia sheria ni bei ndogo sana kulipia itikadi muhimu kama Demokrasia na utawala wa Sheria,” amesema Fatma

Jana, Mahakama Kuu iliamuru Fatma asiendelee kuwa wakili kwa muda, kutokana na upande wa serikali kulalamikia matamshi aliyotoa  katika kesi iliyofunguliwa na Ado Shaibu, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa ACT Wazalendo dhidi ya Rais Magufuli  na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Dk. Biteko: Viongozi tuache alama nzuri katika utendaji wetu

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari za SiasaTangulizi

Chanzo maporomoko yaliyoua 65 Hanang, chatajwa

Spread the loveSERIKALI imesema kumeguka kwa sehemu ya Mlima Hanang ambao ilikuwa...

Habari za Siasa

Baba yake Ole Sabaya ashinda Uenyekiti CCM – Arusha

Spread the loveLoy Thomas Sabaya ambaye ni Baba wa aliyekuwa Mkuu wa...

Habari za Siasa

Serikali yaagiza uchunguzi chanzo maporomoko Hanang

Spread the loveSERIKALI imeagiza uchunguzi ufanyike ili kubaini chanzo cha maporomoko ya...

error: Content is protected !!