Friday , 26 April 2024
Home Kitengo Michezo Kushikiliwa kwa Namungo Angola, Majaliwa atoa neno
MichezoTangulizi

Kushikiliwa kwa Namungo Angola, Majaliwa atoa neno

Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu wa Tanzania
Spread the love

 

SAA chache mara baada ya msafara wa Namungo kuzuiliwa kwenye Uwanja wa ndege wa Luanda Angola, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema kuwa jambo hilo limeshawafikia na litawashughulikiwa na Wizara ya Mambo ya Nje. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Majaliwa amesema hayo hii leo tarehe 13 Februari 2021, wakati wa hotuba yake ya kuhailisha mkutano wa pili, kikao cha 10 cha bunge la 12, jijini Dodoma.

Katika hotuba yake Majaliwa kwenye upande wa michezo alianza kuipongeza timu ya Namungo FC kwa kufanikiwa kuingia katika raundi ya tatu kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika na kuwatakiwa kila la kheri kwenye mchezo wao wa kesho dhidi ya Costo De Agosto.

Majaliwa aliendelea kusema kuwa licha ya kuwatakiwa mema kwenye mchezo wao wa kesho lakini wamepata taarifa ya kuwa timu hiyo inashirikiliwa nchini Angola na kueleza kuwa suala hilo linashughulikiwa na serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Nje.

“Naipongeza sana timu ya namungo Fc, kwa kufanikiwa kuvuka hatua mbili za awali kuelekea kwenye makundi kombe la shirikisho Afrika, lakini pia niwatakie kila la kheri kwenye mchezo wao wa kesho huko Angola, ingawa timu hiyo mpaka sasa inashikiliwa na jeshi la nchini Angola ikiwa ni Siasa za kimichezo”

“Sisi kama Tanzania kupitia Wizara ya mambo ya nje tunalifanyia kazi swala hilo ili timu hiyo iweze kushiliki michezo na iweze kurudi nyumbani” alisema Waziri Mkuu

Aidha Majaliwa hakuwa nyuma kuipongeza klabu ya Simba mara baada ya kupata ushindi kwa bao 1-0, kwenye mchezo wa kwanza wa kundi A wa Ligi ya mabingwa Afrika dhidi ya AS Vita Club kutoka Congo DR.

Namungo ambayo imesafiri nchini Angola kwa ajili ya mchezo wa raundi ya tatu wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Costo De Agosto ya nchini Angola.

Mara baada ya kufika Uwanja wa ndege wa Luanda uliopo nchini humo kikosi hiko kilizuliwa kwa madai kuwa wachezaji watatu pamoja na kiongozi wao mmoja wamebainika kuwa na virusi vya Corona.

Maafisa wa nchini humo waliwata msafara wa Namungo FC kwenda karantini au kurejea nchini Tanzania mara moja hali iliyozua sintofahamu na kusalia kwenye Uwanja wa ndege huo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Michezo

EPL, Ligue 1 na Coppa Italia kinawaka leo

Spread the love  LEO ligi kadhaa zitaendelea nchini barani ulaya ikiwemo ligi...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

BiasharaMichezo

NBC yaunga mkono jitihada kutokomeza malaria

Spread the loveKuelekea Maadhimisho ya siku ya malaria Duniani yatakayofanyika kesho Aprili...

error: Content is protected !!