May 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

TFF: Walichofanyiwa Namungo ni kinyume na utaratibu

Kikosi cha timu ya Namungo wakati wakiondoka nchini Tanzania

Spread the love

 

SHIIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limesema kuwa kitendo cha timu ya Namungo FC kutaka kuwekwa karantini nchini Angola baada ya kufanyiwa vipimo vya corona ni kinyume cha utaratibu ya mashindano hayo. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Namungo iliwasili nchini Angola kwa ajili ya kucheza mchezo wa mzunguko wa tatu wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Costo De Agosto, uliopangwa kucheza kesho tarehe 14 Februari 2021.

Taarifa iliyotolewa na TFF imeeleza kuwa kitendo cha mamlaka za Angola kutaka timu nzima iwekwe karantini jeshini ni kinyume na uataratibu wa mashindano ya Shirikisho la Mpira Afrika (CAF) na TFF imefanya mawasiliano ya karibu na shirikisho hilo ili kupata ufumbuzi wa haraka.

Taratibu za CAF kwenye michuano hiyo juu ya corona zinaeleza kuwa timu zitafanyiwa vipimo siku moja kabla ya mchezo na maofisa wa afya kutoka CAF na kama kuna wachezaji watabainika kuwa na virusi hivyo hawatashiriki katika mchezo husika ila ambao watakuwa wazima watacheza.

Wakati TFF ikichukua hatua hiyo tayari Serikali ya Tanzania kupitia Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema kuwa suala hilo la kushikiliwa kwa timu ya Namungo na jeshi la Angola litafuatiliwa kwa karibuni na serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Nje.

“Sisi kama Tanzania kupitia Wizara ya Mambo ya Nje tunalifanyia kazi swala hilo ili timu hiyo iweze kushiriki michezo na iweze kurudi nyumbani,” alisema Majaliwa.

error: Content is protected !!