Thursday , 23 March 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Kukamatwa Mbowe: Prof. Lipumba “Rais Samia hatokwepa lawama”
Habari za Siasa

Kukamatwa Mbowe: Prof. Lipumba “Rais Samia hatokwepa lawama”

Prof. Ibrahim Lipumba
Spread the love

 

MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi (CUF), Prof. Ibrahim Lipumba, amesema Rais Samia Suluhu Hassan, hawezi kukwepa lawama kufuatia tukio la kukamatwa kwa Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Prof. Lipumba ametoa kauli hiyo leo tarehe 23 Julai 2021, siku mbili baada ya Mbowe kukamatwa akiwa hotelini jijini Mwanza, akijiandaa kushiriki kongamano la kudai katiba mpya, lililoandaliwa na Chadema.

Mbowe alikamatwa na wenzake 11, katika Hoteli ya Kingdom jijini Mwanza, usiku wa kuamkia tarehe 21 Julai 2021, kwa tuhuma za kufanya mikusanyiko isiyo halali, kufuatia hatua yao ya kuandaa kongamano hilo.

“Tunatahadharisha kwamba, vitendo hivi visipodhibitiwa mapema vinaweza kuleta shida na Rais Samia hatokwepa lawama,”

“Kwa kuwa mikutano ya hadhara na makongamano ambayo Serikali anayoiongoza inavizuia, vimeruhusiwa na katiba na sheria zingine za nchi alizoapa kuzilinda,” amesema Prof. Lipumba.

Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema

Baada ya kukamatwa na Jeshi la Polisi jijini Mwanza, Mbowe alipelekwa katika Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, anakoshikiliwa hadi sasa kwa tuhuma za ugaidi.

Akizungumzia tuhuma hizo, Prof. Lipumba amehoji kwa nini jeshi hilo halikumkamata kabla ya kongamano hilo kufanyika.

“Jeshi la Polisi lingeweza kumkamata Mbowe popote hata alipokuwa msibani, kama kweli kuna tuhuma zozote dhidi yake. Kumkamata kufuatia kongamano lao la Mwanza na kisha kudai kwamba anatuhumiwa kwa ugaidi, ni jambo linaloibua maswali mengi bila majibu,” amedai Prof. Lipumba.

Prof. Lipumba ameiomba Serikali imuachie huru Mbowe na wenzake, waliokamatwa jijini Mwanza, wakijiandaa kufanya kongamano la kudai katiba mpya.

“CUF kinatoa wito kwa Serikali kupitia Jeshi la Polisi, kuwaachia viongozi wote wa Chadema wanaoshikiliwa kufuatia Kongamano la Mwanza,” amesema Prof. Lipmba.

Rais Samia Suluhu Hassan

Mbali na Mbowe, wengine waliokamatwa ni Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha) Taifa, John Pambalu. Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho, John Heche na Mhadhiri Mstaafu, Dk. Azaveli Lwaitama.

Nje ya CUF, Chama cha ACT-Wazalendo na NCCR-Mageuzi, vimetoa tamko la kupinga kukamatwa kwa Mbowe.

Hata hivyo, Msemaji Mkuu wa Serikali ya Tanzania, Gerson Msigwa, amewataka watu wanaopinga uamuzi huo kuliacha Jeshi la Polisi lifanye kazi yake.

“Kila nchi zina taratibu zake, tuliachie Jeshi la Polisi lifanye kazi yake, likimaliza litatueleza,” amesema Msigwa.

2 Comments

  • Matatizo ya nchi za kiafrika yanatokana na viongozi wa Afrika kwa kulewa madaraka na kujifanya waungu watu kwa kuwaburuza raia kama takataka za (mashudu) huku wao na na kikundi cha familia zao wakitaka kubakia madarakani kana kwamba wamekalia kiti chenye gundi ambalo hawawezi kubanduka.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Samia aagiza iundwe kamati ya pamoja ya Mawaziri mradi wa BBT

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amewaagiza mawaziri kuunda kamati...

Habari za Siasa

Rais Samia apangua makatibu tawala mikoa, ateua Kamishna DCEA

Spread the loveALIYEKUWA Kamishna wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya, Gerald...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

M/kiti bodi ya wadhamini Chadema afariki dunia

Spread the loveMWENYEKITI wa Bodi ya Wadhamini ya Chama cha Demokrasia na...

Habari za Siasa

Zitto: Nikifa Ado atavaa viatu vyangu

Spread the love  KIONGOZI Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe...

error: Content is protected !!