Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Majaliwa awatangazia neema watumishi umma
Habari za Siasa

Majaliwa awatangazia neema watumishi umma

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
Spread the love

 

WAZIRI Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan imedhamiria kuboresha maslahi ya watumishi wa umma nchini wakiwemo waalimu, hivyo amewataka wafanye kazi kwa bidii na maarifa. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Majaliwa aliyasema hayo jana Ijumaa, tarehe 23 Julai 2021, wakati akizungumza kwa nyakati tofauti na wananchi wa wilaya ya Ruangwa kwenye mikutano ya hadhara iliyofanyika katika kijiji cha Chinokole na Shule ya Sekondari ya Kassim Majaliwa.

Alisema licha ya kuboresha maslahi ya watumishi pia Serikali imeendelea kuimarisha miundombinu mbalimbali ikiwemo ya sekta ya elimu kama ujenzi wa vyumba vya madarasa, maabara, matundu ya vyoo na nyumba za walimu katika shule za msingi na sekondari nchini.

Rais Samia Suluhu Hassan

Majaliwa alisema lengo la maboresho hayo ni kuhakikisha wanafunzi wanasoma katika mazingira bora yatakayowafanya wapende masomo na kuongeza ufaulu.

“Pia tunajenga mabweni ili kuwawezesha wanafunzi kukaa shuleni na kupata muda mwingi wa kujisomea,” alisema.

Kadhalika, Majaliwa alitumia fursa hiyo kuwasisitiza Watanzania waendelee kushikamana na kushirikiana na Serikali yao kwa kushiriki katika shughuli mbalimbali za maendeleo kwa ajili ya manufaa yao binafsi na Taifa kwa ujumla.

Pia, Waziri Mkuu alikagua miundombinu ya shule ya Sekondari ya Kassim Majaliwa ukiwemo mradi wa ujenzi wa nyumba za walimu ambapo alisema ameridhishwa na mradi huo na kuwataka waliokabidhiwa jukumu la kusimamia wahakikishe mradi huo unakamilika kwa wakati.

Wakati huo huo, Waziri Mkuu alisema Serikali imeadhamiria kuwekeza katika elimu ya mtoto wa kike kwa lengo la kumuwezesha kutimiza ndoto zake kielimu.

“Tunataka watoto wa kike wasome bila usumbufu ili waweze kutimiza ndoto zao,” alisema.

Katika kuhakikisha jambo hilo linafanikiwa, Majaliwa alisema Serikali imeanzisha mradi wa ujenzi wa shule za wasichana kwenye maeneo mbalimbali nchini pamoja na kwenye wilaya ya Ruangwa ili kutoa nafasi nzuri kwa mtoto wa kike kupata fursa ya kusoma vizuri akiwa katika mazingira rafiki yatakayo muepusha na changamoto zinazowafanya washindwe kutimiza malengo yao kielimu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Dk. Mwakyembe : Zanzibar waliongoza kutaka Serikali 2 za muungano

Spread the love  MWANASIASA mkongwe nchini, Dk. Harrison Mwakyembe, amesema mjadala wa...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia ataja mikakati ya kufikia trilioni 2 biashara Uturuki, Tz

Spread the loveWakati Tanzania na Uturuki zikidhamiria kuongeza kiwango cha biashara hadi...

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

error: Content is protected !!