July 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kisa Simba, Yanga yapigwa faini ya mil 3

Spread the love

 

KLABU ya Soka ya Yanga, imepigwa faini ya Shilingi milioni tatu, mara baada ya kufanya makossa manne kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Simba uliofanyika Jumamosi ya tarehe 3 julai 2021, kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Yanga imepigwa faibi hiyo mara baada ya kutumia mageti ya uwanja wa Uhuru walipoingiza timu kwenye Uwanja wa Mkapa, badala ya kupitia geti kubwa, pia klabu hiyo pia imepigwa faini kwa kutumia mlango wa chumba cha waandishi wa habari, badala ya mlango maalumu unaotumia na timu.

Aidha bodi ya Ligi nchini imeitoza tena faini Yanga, kwa kutumia mlango wa gati B, wakati wa timu hiyo ilipoingia Uwanjani kupasha misuli moto, kinyume na utaratibu.

Faini nyingine kwa Yanga, ilikuja mara baada ya kutumia chumba cha wafanya usafi kubadilishia nguo, badala ya kutumia vyumba maalumu vilivyopangwa.

Bodi hiyo pia imewataka Yanga kulipa kiasi cha shilingi 850,000 ikiwa gharama ya ukarabati wa mageti yaliyovunjwa wakati wakiingiza timu hiyo Uwanjani.

Kwenye mchezo huo Yanga, ilifanikiwa kuibuka na Ushindi wa bao 1-0, lililofungwa kwenye dakika ya 12 na Zawadi Mauya.

error: Content is protected !!