Sunday , 29 January 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Kinana: Wasio tutakia mema wanatutoa kwenye ajenda muhimu
Habari za Siasa

Kinana: Wasio tutakia mema wanatutoa kwenye ajenda muhimu

Abdulrahman Kinana, Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara
Spread the love

 

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana, amesema wasiokitakia mema chama hicho wanawatoa kwenye ajenda muhimu na kujikuta wakijadili mambo yasihusu ajenda za wananchi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Kinana ameyasema hayo leo Jumapili tarehe 27, Novemba, 2022, wakati akifungua Mkutano Mkuu wa 10 wa Jumuiya ya Vijana UVCCM, jijini Dodoma.

“Wasio tutakia mema huwa wanatutoa kwenye ajenda muhimu na sisi kwasababu hatujiandaa tunafuata mkumbo na kuanza kujadili mambo ambayo hayana uhusiano wa moja kwa moja na mambo ambayo tumeahidi Watanzania, amesema Kinana.

Amesema kazi mojawapo ya jumuiya ya chama hicho ni kusemea na kutetea chama na Serikali za pande zote za muungano kwa kutumia hoja nzuri ambapo amewataka vijana kusoma ili kupata hoja za kusema na kutetea.

“Hoja hushindwa na hoja bora zaidi na hoja iliyobora zaidi haitoki hewani, haiwezi kubuniwa lazima iwe ni hoja iliyofanyiwa uchambuzi. Wakati mwingine nasoma watu wanavyobishana na huoni uzito mkubwa sana wa mabishano au thamani ya hoja zinazobishaniwa,” amesema Kinana

Katika hatua nyingine Kinana amesema ni uykweli kwamba ndani ya Seriklai ya awamu ya sita fedha nyingi za maendeleo zimepelekwa kwa wananchi na kufanya kazi kuliko kipindi kingine chochote.

“Tangu nimekuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama hiki, nimetembelea mikoa 12… jambo moja ambalo limekuwa dhahiri kwamba fedha nyingi zimetolewa na kazi zimefanyika. Hakuna kipindi ambacho fedha nyingi za maendeleo zimetolewa kama hivi sasa hatusemi kwa kusifia bali huo ndio ukweli wenyewe,” amesema.

1 Comment

  • Hakuna uwazi wa matumizi ya hizo fedha kwa minajiri ya thamani ya mradi. Value for money + impact kwa wananchi wanaolengwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

NCCR-mageuzi yawaangukia Polisi kupotea kwa kada wake

Spread the loveJESHI la Polisi nchini limeombwa kufanya uchunguzi wa kina utakaosaidia...

Habari za Siasa

Uamuzi kesi ya kupinga Bodi ya Wadhamini NCCR-Mageuzi kutolewa Februari 6

Spread the love  MAHAKAMA Kuu, Masjala Kuu ya Dar es Salaam, imepanga...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu:Suluhu ya ugumu wa maisha ni Katiba Mpya

Spread the love  MAKAMU mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo-Chadema Bara,...

Habari za Siasa

Lissu: Miaka 30 ya vyama vingi haikupambwa kwa marumaru

Spread the love  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo-Chadema, Tundu...

error: Content is protected !!