Sunday , 29 January 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Watunza kumbukumbu za umma sasa kula kiapo
Habari za SiasaTangulizi

Watunza kumbukumbu za umma sasa kula kiapo

Rais Samia Suluhu Hassan
Spread the love

 

WATUNZA kumbukumbu na nyaraka za Serikali sasa watalazimika kula kiapo cha maadili ya kazi yao kutokana na kile kilichoelezwa ni unyeti wa taarifa wanazozitunza. Anaripoti Mwandishi Wetu, Arusha … (endelea).

Wazo hilo limetolewa na Mawaziri wa Utumishi bara na Zanzibar na kurudhiwa na Rais Samia Suluhu Hassan ambaye ametangaza utaratibu huo kuanza rasmi mwakani.

Mkuu huyo wa nchi ametangaza utaratibu huo leo Jumapli tarehe 27, Noemba 2022, wakati akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa 10 wa Chama cha Taaluma ya Menejimenti ya Kumbukumbu na Nyraka Tanzania (TRAMPA) unaofanyika jijini Arusha.

“Kwa umuhimu wa kazi yenu ni kweli mnapaswa kula kiapo ingawa hakihakikishi kila kitu, lakini wale wote wanaokwenda kinyume na kiapo walichokula hawafiki mbali kwasababu wanamdhihaki Mwenyezi Mungu,” amesema Rais Samia.

“Sasa tuapishane,” ameongeza.

Pia ametangaza kuwa Mkutano watakaoutumia kula kiapo utafanyika visiwani Zanzibar ambapo amewataka mawaziri wa pande zote kushirikiana katika maandalizi.

“Katika mkutano huo tutakula kiapo pale inshala kwenye uhai na uzima na usalama nami nitakuwepo kwahiyo mawaziri jipangeni huo ni ugeni mkubwa sana anzeni kujipanga kuanzia sasa ni mwezi gani hilo tutapanga,” amesema Rais Samia

Katika hatua nyingine Rais Samia amesisitiza umuhimu wa wataunza kumbukumbu na nyaraka kutunza siri za Serikali kwani kuvujishwa kwa taarifa kunaweza kuleta atahri kubwa katika utendaji wa Serikali na kwenye jamii.

“Ninyi ndiyo roho ya utendaji wa serikali chanzo cha kufanikiwa kwa serikali katika utendaji ni mtunza kumbukumbu,” amesisitiza.

Amesema wakati wa enzi zao za kutunza kumbukumbu hawakuwa na teknolojia kama ilivyo sasa na kwamba mengi walihifdhi kichani na kukumbuka pale yanapohitajika.

“Leo mna makompyuata mnaweka huko lakini mnaweka kwenye makabati hakuna sababu ya kuharibu hakuna sababu kwanini Serikali isifanye kazi bila kupotza nyaraka,” amesema Rais Samia ambaye amewahi kuwa Mtunza Kumbukumbu na Nyaraka katika ofisi za Serikali Zanzibar.

Amesema “kuna mambo yanaonekana kwenye mitandao barua, kesi ilivyohukumiwa kwenye mitandao unajiuliza huyu aliyetoa hizi taarifa anataka umaarufu, rushwa au kitu gani.”

Amesema vitendo hivyo vinaweza kusababisha lolote na kuleta uchonganishi kwa nchi.

Amesisitiza serikali inafanya kazi zake kwa utaratibu na kwamba kutoka nje ya utaratibu haileti picha nzuri.

“Sisi mama zenu hatukufanya hivyo na nawaomba nhyie tunzeni siri za Serikali…nendeni kafanyeni kazi kwa weledi na uadilifu mkubwa,” amesema Rais Samia.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Haya hapa matokeo ya mtihani kidato cha nne 2022

Spread the loveBARAZA la Mitihani la Tanzania (Necta) leo Jumapili limetangaza matokeo...

Habari za Siasa

NCCR-mageuzi yawaangukia Polisi kupotea kwa kada wake

Spread the loveJESHI la Polisi nchini limeombwa kufanya uchunguzi wa kina utakaosaidia...

HabariTangulizi

Bakwata wamkangaa Sheikh wa Dar es Salaam

Spread the love  BARAZA la Ulamaa, limefutilia mbali uamuzi wa “kuvunja ndoa,”...

Habari za Siasa

Uamuzi kesi ya kupinga Bodi ya Wadhamini NCCR-Mageuzi kutolewa Februari 6

Spread the love  MAHAKAMA Kuu, Masjala Kuu ya Dar es Salaam, imepanga...

error: Content is protected !!