Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kina Mbowe wapinga hati ya ukamataji, Jaji aahirisha kesi
Habari za SiasaTangulizi

Kina Mbowe wapinga hati ya ukamataji, Jaji aahirisha kesi

Spread the love

 

UPANDE wa utetezi, katika kesi ya uhujumu uchumi, inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake, wameipinga hati ya kukamatwa watuhumiwa wawili katika kesi hiyo, Adam Kasekwa na Mohammed Abdillah Ling’wenya. Anaripoti Regina Mkonde, Dar ea Salaam … (endelea).

Pingamizi hilo limewekwa na upande wa utetezi katika Mahakama Kuu, Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, mbele ya Jaji Joackim Tiganga, baada ya shahidi wa nane wa Jamhuri, Mkuu wa Upelelezi Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha, ASP Jumanne Malangahe, kuiomba iipokee kama sehemu ya ushahdii wa upande wa mashtaka.

Wakili wa utetezi, Nashon Nkungu, aliweka pingamizi hilo akidai hati hiyo imeletwa kwa sheria ambayo haipo nchini.

Wakili Nkungu amedai, hati hiyo imeletwa mahakamani hapo chini ya kifungu cha 38 (3), cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya jinai, iliyofanyiwa marekebisho 2018, wakati sheria hiyo haipo nchini.

“Hoja yetu hati imechukuliwa kwa sheria ambayo haipo, na hii siyo nyaraka binafsi angeweza andaa anavyotaka, isipokuwa msingi wake ni wa kisheria. Hati hii imepetwa cjini ya kifungu cha 38 (3), cha Sheria ya Mwenenso wa Makosa ya Jinai iliyofanyiwa marekebishi 2018, hakuna sheria hiyo hapa nchini,” amedai Wakili Nkungu.

Naye Wakili Peter Kibatala, ameiomba mahakama hiyo isiipokee hati hiyo akidai haina uhai wa kisheria mahakamani hapo sababu hakuna sheria ya mwenenso wa makosa ya jinai iliyorekebishwa 2018, bali iliyopo ilirekebishwa 2019. Hivyo, mawakili wa jamhuri walipaswa kuieleza mahakama kulikuwa na makosa ya uchapaji.

Kutokana na pingamizi hilo, Jaji Tiganga alielekeza mawakili wa jamhuri wajibu hoja hizo.

Ambapo Wakili wa Serikali Mwandamizi, Robert Kidando, aliomba mahakama hiyo iwape muda wa kupitia hoja za mapingamizi hiyo, ili watoe majibu.

Kufuatia maombi hayo, Jaji Tiganga ameiahirisha kesi hiyo hadi saa 7.20 mchana.

Mapema leo Jumatatu, ASP Jumanne alitoa ushahidi wake namna alivyowapekua watuhumiwa hao, tarehe 5 Agosti 2020, baada ya mukamatwa maeneo ya Rau Madukani, Moshi mkoani Kilimanjaro.

Kwa mujibu wa ASP Jumanne, washtakiwa hao baada ya kupekuliwa, mmoja ambaye ni Kasekwa, alikutwa na simu, silaha aina ya bastola yenye risasi tatu na kete 58 ambazo baadae ziligundulika kuwa ni za dawa za kulevya. Huku mwenzake Ling’wenya alidaiwa kukutwa na kete 25 za dawa hizo pamoja na simu.

Endelea kufuatilia MwanaHALISI TV, MwanaHALISI Online na mitandao yetu ya kijamii kwa habari na taarifa mbalimbali

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

error: Content is protected !!